Siku ya DNA
Siku ya kimataifa ya DNA | |
---|---|
![]() Muundo wa DNA | |
Husheherekewa na | Wanabaolojia na watu wengine |
Tarehe | 25 April |
Siku ya DNA husherehekewa tarehe 25 Aprili kila mwaka kuadhimisha siku ya mwaka 1953, ambapo wanasayansi James Watson, Francis Crick, Maurice Wilkins, Rosalind Franklin na wenzao walichapisha makala katika jarida la Nature juu ya muundo wa DNA. [1][2][3]
Vilevile, mwanzoni mwa Aprili 2003 ilitangazwa kuwa mradi wa seti kamili ya vinasaba (complete genome) vya binadamu ulikuwa karibu sana kukamilika na "mapungufu madogo madogo yaliyosalia yalionekana kuhitaji gharama kubwa sana kuyakamilisha.”[4][5]
Siku ya DNA iliadhimishwa kwa mara ya kwanza nchini Marekani tarehe 23 Aprili 2003 kwa kutangazwa na seneti[6] na baraza la wawakilishi la nchi hiyo.[7] Walakini, walitangaza maadhimisho hayo kwa mwaka huo tu na si kila mwaka. Tangu mwaka 2003 maadhimisho ya siku ya DNA yamekuwa yakiandaliwa na Taasisi ya kitaifa ya utafiti wa Jinomu ya Binadamu (NHGRI) kuanzia 23 Aprili 2010, 25 Aprili 2011 [8] na 20 Aprili 2012.[9] Tokea hapo tarehe 25 Aprili ilitangazwa rasmi kuwa “Siku ya kimataifa ya DNA”[10][11] na “Siku ya DNA Duniani”[12] [13][14] ambayo imekuwa ikiadhimishwa na vikundi mbalimbali.
Kampuni za upimaji wa DNA na wachapishaji wa majarida ya elimu ya vinasaba huendesha minada ya kila mwaka karibu na maadhimisho ya siku ya DNA wakihamasisha umma na kukuza uelewa kuhusiana na huduma zao.[15]
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Watson, James Dewey; Crick, Francis Harry Compton (1953-04-25). "Molecular structure of nucleic acids; a structure for deoxyribose nucleic acid". Nature 171 (4356): 737–738. . . http://www.nature.com/nature/dna50/watsoncrick.pdf.
- ↑ Franklin, Rosalind Elsie; Gosling, Raymond (1953-04-25). "Molecular configuration in sodium thymonucleate". Nature 171 (4356): 740–741. . . http://www.nature.com/nature/dna50/franklingosling.pdf.
- ↑ Wilkins, Maurice Hugh Frederick; Stokes, Alexander Rawson; Wilson, Herbert R. (1953-04-25). "Molecular structure of deoxypentose nucleic acids". Nature 171 (4356): 738–740. . . http://www.nature.com/nature/dna50/wilkins.pdf.
- ↑ Noble, Ivan. "Human genome finally complete", BBC News, 2003-04-14.
- ↑ International Human Genome Sequencing Consortium (2004-10-21). "Finishing the euchromatic sequence of the human genome". Nature 431 (7011): 931–945. . .
- ↑ A concurrent resolution designating April 2003 as "Human Genome Month" and April 25 as "DNA Day".. United States Government Printing Office (2003-02-27).
- ↑ Recognizing the sequencing of the human genome as one of the most significant scientific accomplishments of the past one hundred years and expressing support for the goals and ideals of Human Genome Month and DNA Day.. Library of Congress. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-10-07. Iliwekwa mnamo 2021-04-23.
- ↑ Join us April 15 for National DNA Day!. National Human Genome Research Institute (2011-04-11).
- ↑ DNA Day 12. National Human Genome Research Institute (2011-11-28).
- ↑ International DNA day to be celebrated. Biotechnology Society of Nepal (2009-06-15).
- ↑ Finley, Erica (2011-04-21). Celebrate International DNA Day in Huntsville. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-04-21. Iliwekwa mnamo 2021-04-23.
- ↑ Annual International DNA Day at the University. Vilnius University (2009-04-06).
- ↑ International Consortium Publishes Sequence, Analysis Of The Human Genome. World High Technology Society. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-07-21. Iliwekwa mnamo 2021-04-23.
- ↑ Genomes, Environments and Traits Conference. GET Conference.
- ↑ MacEntee, Thomas (2019-04-23). Best Promo Codes, Coupons and Savings on DNA during National DNA Day Sale (en-US). Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-02-25. Iliwekwa mnamo 2021-04-23.