Sigara ya elektroniki
Sigara ya elektroniki ni kifaa cha elektroniki cha mkononi kinachojaribu kujenga hisia za sigara ya tumbaku.
Inafanya kazi kwa kutoa mvuke ambao huvutwa na mtumiaji. Mvuke huo mara kwa mara hubeba nikotini, propelini, glaserini, na ladha za aina mbalimbali. Hata hivyo, si sigara zote za aina hii zina nikotini.
Sigara ya kwanza ya elektroniki ilitoka Uchina; mganga Mchina Han Lok, mwenye miaka 57 ndiye aliyetengeneza hiyo sigara.
Bado kuna utata kuhusu hatari za afya za sigara hiyo, lakini kwa ujumla zinachukuliwa kama ni salama kuliko sigara za tumbaku. Inaaminika pia kuwa zinaweza kusaidia wavutaji wa sigara ya tumbaku kuacha, ila wengine wanasema zinajenga uraibu mwingine.
Tahadhari imetolewa kwa wale wanaonunua bangi mitaani na kuitumia katika uvutaji wa vifaa hivi. Kutokana na teknolojia ya uchomaji ndani ya vifaa hivi kuwa tofauti na uchomaji wa sigara za kawaida, kuna matone ya mafuta ya bangi hubaki bila kuwa mvuke, hivyo mvutaji huishia kuyavuta hayo mafuta na kuyaingiza kwenye mapafu, huku akijisababishia athari mbaya kiafya na uwezekano wa kupoteza uhai[1].
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Outbreak of Lung Illness Associated with Using E-cigarette Products". Centers for Disease Control and Prevention. 6 September 2019
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sigara ya elektroniki kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |