Nenda kwa yaliyomo

Sidibé Aminata Diallo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sidibé Aminata Diallo (alizaliwa 1950) ni msomi na mwanasiasa kutoka Mali[1].Yeye ni profesa wa mipango miji katika Chuo Kikuu cha Bamako na amewahi kufanya kazi katika UNESCO.[2]

Diallo alipata shahada yake ya udaktari katika maendeleo na masomo ya mjini kutoka Chuo Kikuu cha Toulouse mwaka wa 1984[1].Ni mwanachama wa kitivo cha Sayansi ya Kiuchumi na Usimamizi katika Chuo Kikuu cha Bamako, ambapo ni mtaalamu wa usimamizi wa ardhi.[3]

Tarehe 12 Machi 2007, Diallo alitangaza kugombea nafasi ya Uraisi.Alikuwa mmoja wa wagombea 8 walioshiriki uchaguzi wa urais wa Aprili 2007.Pia alikuwa mgombea urais wa kwanza mwanamke kuwahi kutokea nchini Mali, na alikuwa akigombea kama mgombea wa 'Harakati za Elimu ya Mazingira na Maendeleo Endelevu'. Nia yake kuu ni uendelevu na ulinzi wa mazingira. Diallo alipata zaidi ya kura 12,000 katika uchaguzi, 0.55% ya jumla ya kura.

Kufuatia uchaguzi huo, Diallo aliteuliwa kuwa Waziri wa Elimu ya Msingi, Kusoma na Kuandika na Lugha za Kitaifa tarehe 3 Oktoba 2007.[4] Alishikilia wadhifa huo hadi nafasi yake ilipochukuliwa na Salikou Sanogo tarehe 9 Aprili 2009.[5]

  1. 1 2 Imperato, Pascal James; Imperato, Gavin H. (2008-04-25). Historical Dictionary of Mali (kwa Kiingereza). Bloomsbury Publishing PLC. ISBN 978-0-8108-6402-3.
  2. News Agencies. "Mali votes in presidential poll". Al Jazeera (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-07.
  3. "allAfrica.com: Mali: A Presidential Election That Breaks With Tradition". allafrica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-07.
  4. "allAfrica.com: Mali: Amadou Toumani Touré remanie". fr.allafrica.com (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2025-10-07.
  5. "Students left behind in race for education MDG". www.thenewhumanitarian.org (kwa Kiingereza). 2009-02-06. Iliwekwa mnamo 2025-10-07.