Shore (Pycnonotidae)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shore
Shore tako-njano
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Pycnonotidae (Ndege walio na mnasaba na shore)
G.R. Gray, 1840
Ngazi za chini

Jenasi 9 za shore:

Shore, shorwe au sholwe ni ndege wadogo wa familia Pycnonotidae ambayo ina korogoto na nyembelele vilevile. Spishi za nusufamilia Muscicapinae zinaitwa shore pia.

Wale wa Pycnonotidae wana rangi ya kahawia au kijivu, pengine nyeusi, na kwa kawaida nyeupe chini. Spishi nyingine zina rangi kali kama buluu na nyekundu. Spishi nyingi zina kishungi.

Shore wanatokea misitu na maeneo mengine yenye miti katika Afrika na Asia. Tago lao hujengwa mtini na jike hutaga mayai 2-5.

Hula matunda na mbegu hasa, lakini wadudu pia.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za Asia[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]