Nenda kwa yaliyomo

Shishiyu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Shishiyu ni kata ya Wilaya ya Maswa, tarafa ya Malampaka, katika Mkoa wa Simiyu, Tanzania, yenye postikodi namba 39326 [1].

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 15,582 [2]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 24,695 waishio humo.[3].

Wenyeji wa kata hii ni Wasukuma wakarimu, wenye urafiki, wapenda wageni na wasiokuwa na makuu, ambao hujishughulisha na kazi za kilimo cha mazao kama vile: mpunga, mahindi, pamba, karanga, mtama na maharage; ufugaji wa ng'ombe, mbuzi, kuku, bata na kondoo; biashara, shughuli za kiutawala na kazi za ofisini.

Hali ya hewa ya Shishiyu ni nzuri kwani si joto sana wala baridi sana. Hali hii imechangia kuwa na mwingiliano wa watu wa maeneo mbalimbali ambao hushawishika kuhamia Shishiyu kuishi, kujishughulisha na biashara ya kununua mazao ya mpunga na pamba ambayo huzalishwa kwa wingi.

Lakini zaidi mji wa Shishiyu umeunganishwa na miundombinu imara ya barabara, hivyo unafikika kwa urahisi. Iwe kutoka Mwanza, Shinyanga, makao makuu ya mkoa, wilaya ya Maswa na wilaya ya Magu usafiri upo na wa uhakika.

Kata hii imebarikiwa kuwa na mwamko mzuri wa kielimu, kwani wakazi wake wana bidii sana ya kusomesha watoto wao. Kata hii ina shule mbili za sekondari, yaani: Shule ya Sekondari ya Shishiyu na Shule ya Sekondari ya Jija. Shule ya sekondari ya Shishiyu tangu kuanzishwa kwake imekuwa na mafanikio makubwa sana katika elimu, ikifaulisha wanafunzi wengi kila mwaka katika mitihani yake ya wilaya, ya mkoa, na ya kitaifa. Licha ya kuwa iko nje ya makao makuu ya wilaya, imekuwa kivutio kikubwa kwa vijana wa maeneo mbalimbali, kwa mfano Maswa mjini, Malampaka, Bariadi n.k. Hali hiyo imechangia mafanikio makubwa kwa Wanashishiyu wote kupenda elimu.

Lakini pia penye maendeleo hapakosi kuwa na changamoto mbalimbali; kama vile uongozi mbaya, rushwa, ukosefu wa maji safi na salama, licha ya kuwa kata ya kwanza inayokua kwa kasi na yenye mafanikio zaidi ya kitaaluma katika kata zote za wilaya ya Maswa.

  1. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
  2. https://www.nbs.go.tz, uk 221
  3. Sensa ya 2012, Simiyu Region - Maswa District Council
Kata za Wilaya ya Maswa - Mkoa wa Simiyu - Tanzania

Badi | Binza | Buchambi | Bugarama | Budekwa | Busangi | Busilili | Dakama | Ipililo | Isanga | Jija | Kadoto | Kulimi | Lalago | Malampaka | Masela | Mataba | Mbaragane | Mpindo | Mwabaratulu | Mwabayanda | Mwamanenge | Mwamashimba | Mwang'honoli | Nguliguli | Ng'wigwa | Nyabubinza | Nyalikungu | Sangamwalugesha | Senani | Seng'wa | Shanwa | Shishiyu | Sola | Sukuma | Zanzui


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Simiyu bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.