Nenda kwa yaliyomo

Shirika la Ulaya la Utafiti wa Nyuklia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nembo ya CERN
Nchi zinazounda Shirika la Ulaya la Utafiti wa Nyuklia (CERN).

CERN (kifupi cha jina la Kifaransa: Conseil Européen pour la Recherche Nucléaire; kwa Kiswahili: Shirika la Ulaya la Utafiti wa Nyuklia) ni shirika la kimataifa na maabara kubwa zaidi duniani kwa ajili ya fizikia ya chembe (particle physics). Makao makuu yake yapo Meyrin, karibu na Geneva, kwenye mpaka wa Uswisi na Ufaransa.

Shirika hili lilianzishwa mwaka 1954 na lina nchi 23 kutoka Ulaya na kote duniani. CERN inajulikana sana kwa kuwa na mashine ya Large Hadron Collider (LHC) na pia kama mahali ambapo Wavuti wa Walimwengu (World Wide Web) ulibuniwa na Tim Berners-Lee mwaka 1989.

Pia, CERN inasimamia mfumo wa Zenodo kwa ajili ya kuhifadhi data za utafiti wa kisayansi.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]