Shirika la Huduma za Maktaba Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Shirikia la Huduma za Maktaba Tanzania (kwa Kiingereza "Tanzania Library Services Board" au kifupi TLSB) lilianzishwa kisheria chini ya sheria za Tanzania iliyopitishwa na bunge mwaka 1972.

Shirika la Huduma za Maktaba Tanzania limekabidhiwa jukumu la kusimamia maendeleo ya huduma za maktaba Tanzania ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri, kutoa mafunzo ya ukutubi kwa ngazi ya cheti na stashahada.

Shirika hili la umma linafanya kazi chini ya Wizara ya Elimu Tanzania na limesambaa katika mikoa yote Tanzania isipokuwa mkoa wa Singida peke yake. Lipo pia katika wilaya 33 za Tanzania bara.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]