Nenda kwa yaliyomo

Shirika la A.H. Belo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shirika la A.H. Belo
Nembo ya Shirika la AH Belo
Jina la kampuni Shirika la A.H. Belo
Ilianzishwa Dallas, Texas
kutoka kampuni ya ,hapo awali, Belo
Huduma zinazowasilishwa Uchapishaji
Mmiliki Robert W. Decherd
Mkurugenzi Mkuu
Rais
Mwenyekiti
Aina ya kampuni Kampuni ya Umma
Makao Makuu ya kampuni Dallas , Texas
Marekani Marekani
Bidhaa zinazosambazwa na kampuni hii Magazeti
Nchi Marekani
Tovuti http://www.ahbelo.com/
ofisi kuu ya shirika

A.H Belo Corp ni kampuni inayohusika na vyombo vya habari iliyokuwa na makao yake Dallas,Marekani. Kampuni hii inamiliki magazeti manne ya kuchapishwa kila siku na majarida matano madogomadogo. Shirika la sasa liliundwa baada ya Shirika la Belo kugawanya operesheni zake za utangazaji na za uchapishaji kuwa mashirika mawili. Mkurugenzi mkuu ni Robert Decherd ambaye alikuwa akiongoza Shirika la Belo kabla ya mgawanyiko huo kufanyika. Makao makuu ya kampuni hii ni Jengo la Belo Building katika eneo la Dallas.

Kampuni hii ilianzishwa kama shirika dogo lililomilikiwa na Shirika la Belo mnamo 1 Oktoba 2007. Mnamo 8 Februari 2008 hisa za kampuni ziliuzwa kwa umma ili watu wapate kumiliki kampuni hii. Ingawa kampuni hii ilianzishwa katika mwaka wa 2008, shirika hili lina mizizi yake na historia yake kutoka mwaka wa 1842. Shirika la Belo lilitumia jina la A.H. Belo kutoka mwaka wa 1926 hadi mwaka wa 2002 lilipofupishwa kuwa Belo. Mgawanyiko wa shirika hili liliwapa nafasi ya kutumia jina la zamani ambalo ni linatumika kwa makumbusho ya Alfred Horatio, mwanzilishi wa Dallas Morning News.

Magazeti

[hariri | hariri chanzo]

o Al Día (Lugha ya Kihispania - Dallas, Texas) o Quick (gazeti la kila wiki la bure linalochapishwa na Dallas Morning News - Dallas, Texas)

o Business Press (Riverside, California) o The Difference Desert Daily (Riverside, California) o La Prensa en Linea (Lugha ya Kihispania - Riverside, California)

  1. "Contact Us." Archived 6 Februari 2010 at the Wayback Machine. A. H. Belo.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]