Nenda kwa yaliyomo

Shikoh Gitau

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Shikoh Gitau (alizaliwa 1981) ni mwanasayansi wa kompyuta kutoka nchini Kenya. Alimaliza masomo yake ya shahada ya kwanza ya Sayansi ya Kompyuta kutoka chuo kikuu cha Africa Nazarene University na kupata shahada ya Uzamili kutoka University of Cape Town.[1]

Anajulikana kwa kubuni programu za simu za mkononi za M-Ganga na Ummeli, zinazolenga kuhamasisha afya na tiba pamoja na kuwaunganisha watu wasio na ajira na fursa za kazi. Gitau alikuwa Mwafrika wa kwanza kushinda ufadhili wa Google Anita Borg Memorial Scholarship, uliotolewa katika Grace Hopper Celebration of Women in Computing, kutokana na ubunifu na tasnifu yake.[2]

Hadi Agosti 2017, alichangia na kusimamia mpango wa Technology Innovations for Inclusive Growth katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).[3]

Kwa sasa, Dkt. Shikoh Gitau anahudumu kama Afisa Mkuu Mtendaji (CEO) wa Qhala, kampuni ya teknolojia inayohusika katika mageuzi ya kidijitali barani Afrika, ambayo aliianzisha mwaka 2020.[4][5]

  1. "Genius who captured Google's heart". The Standard (Kenya). Desemba 25, 2010. Iliwekwa mnamo Machi 5, 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Rottok, KC (Mei 30, 2011). "Shikoh Gitau: First African to receive a Google Award". The African Professional. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Machi 8, 2018. Iliwekwa mnamo Machi 5, 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Shikoh Gitau". HuffPost. Iliwekwa mnamo Machi 5, 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "From Mathare slum to Kenya's Covid war room". Daily Nation (kwa Kiingereza). 2021-06-21. Iliwekwa mnamo 2025-04-25.
  5. "Milestone as Qhala launches Africa AI Declaration at Global Summit". The Star (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-04-25.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shikoh Gitau kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.