Shikamoo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Shikamoo ni neno linalotumiwa kumsabahi mtu. Ni salamu inayotumiwa na wadogo kwa wakubwa wao, hasa wale wanaowazidi umri.

Jibu lake ni "Marahaba".

Maana ya neno huelezwa kuwa kifupi cha "nashika mguu wako" kama tamko la heshima mbele ya mkubwa.

Jibu la "marahaba" ni salamu ya Kiarabu inayotumiwa kati ya Waarabu sawa na "hujambo", ila kwa matamshi ya "marhaba". Pale jibu ni "marhabteen" yaani marhaba mara mbili.

Matumizi yake ni kawaida katika Kiswahili nchini Tanzania, huko Kenya mara nyingi haieleweki isipokuwa kwenye maeneo ya pwani.

Blank template.svg Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shikamoo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.