Sheria ya Uingereza

Sheria ya Uingereza (pia huitwa common law) ni mfumo wa sheria wa Uingereza na Wales. Kwa kawaida hugawanywa katika sheria ya jinai na sheria ya kiraia. Mfumo huo ulienea katika sehemu nyingi za zamani za Milki ya Britania ikiwa ni pamoja na Australia, Kanada (isipokuwa Quebec ambayo hutumia sheria ya kiraia), Marekani (isipokuwa Louisiana ambayo hutumia sheria ya kiraia) na New Zealand, pamoja na nchi nyingine nyingi.[1] Kuna takribani nchi 80 duniani zinazotumia mifumo ya sheria ya common law kwa kiasi kikubwa.[2] Takribani nchi 150 hutumia mfumo wa sheria ya kiraia.[2]
Sheria ya Uingereza ni ya kipekee kwa kuwa inategemea matumizi ya kesi zilizopita katika kufanya maamuzi ya sasa na yajayo.[1] Hakimu analazimika kufuata maamuzi ya zamani yaliyofanywa na mahakama za juu lakini si lazima afuate yale ya mahakama za chini.[1] Sheria ya Kiingereza haina katiba na hakuna msimbo rasmi wa kisheria.[3] Hata hivyo, kuna machapisho yasiyo rasmi yanayotoa orodha zilizopangwa za sheria za sasa.[3] Bunge lina mamlaka ya kutunga sheria ambazo huchukuliwa kuwa halali moja kwa moja na haziwezi kupitiwa upya na mahakama.[3] Ni Bunge pekee lina uwezo wa kubadilisha sheria.[3]
Historia
[hariri | hariri chanzo]
Sheria ya Æthelberht (Athelbert wa Kent), iliyoandikwa karibu 602, ni mfano wa kale zaidi wa sheria za Kianglo-Saksoni,[4] au ya sheria katika lugha yoyote ya Kijerumaniki. Sheria za Kianglo-Saksoni zilitegemea sheria za kale za Kijerumani ambazo zilikuwa mfumo wa sheria uliotegemea undugu wa damu.[5] Kundi la undugu lilikuwa na jukumu la matendo ya wanachama wake na pia ulinzi wao. Mdhulumu alitakiwa kulipa Weregild[6], thamani iliyowekwa kwa kila mtu na mali.[5] Kufikia karne ya 10, mfumo huo ulibadilika kuwa wa hundreds.[5] Mfumo huo mpya haukutegemea tena undugu bali ulijipanga kulinda watu na kutekeleza sheria.[5] Mtu aliyeitwa hundredsmann alikuwa na jukumu la kusimamia sheria katika eneo hilo.[5]
Mnamo 1066, Uvamizi wa Wanormani nchini Uingereza ulileta mabadiliko mengi katika sheria.[7] Ingawa sehemu kubwa ya sheria za Anglo-Saxon zilibaki, sheria mpya ziliongezwa na Wanormani.[7] Kabla ya uvamizi wa Norman, sheria nyingi zilikuwa za eneo na zinatekelezwa na mahakama za eneo.[8] Mahakama za kifalme ziliingizwa[8] na ziliweka sheria hizi mpya taratibu.[8] Mahakama za kifalme zilichukua sheria bora za maeneo mbalimbali na kuzieneza nchini kote.[8] Hii iliunda common law ya Kiingereza, yaani mfumo wa sheria sawa kwa taifa zima.[8] Wakati huo, mfumo mwingine wa mahakama ulianzishwa uliojulikana kama equity chini ya Court of Chancery (Mahakama ya Haki au Usawa).[1] Equity ilihusika na kesi ambazo common law haikuzishughulikia. Mfano wa maamuzi ya equity ni kuweka lien[9], kusahihisha mipaka ya ardhi au kuamuru mtu afanye jambo ili kuzuia madhara.[10]
Karne ya 18 mtaalamu wa sheria William Blackstone aliandika kazi ya juzuu nne iitwayo Commentaries on the Laws of England ambayo kwa mara ya kwanza ilitoa muhtasari wa sheria ya Kiingereza.[11] Ilichapishwa kati ya 1765–1769, na imeshachapishwa tena mara nyingi.[11] Kazi hii ilitumika kufundishia sheria hadi karne ya 19 nchini Uingereza na Marekani.[11] Abraham Lincoln alisoma kazi hii akiwa anajifundisha sheria mwenyewe.[12]
Mfumo wa majaji wa wazee (jury system)
[hariri | hariri chanzo]Mfumo wa majaji huenda uliingia Uingereza baada tu ya uvamizi wa Norman.[13] Kwanza, wajumbe walikuwa mashahidi wa mahakama, lakini baadaye, hadi kipindi cha Henry II wa Uingereza, waligeuka kuwa wapambanuzi wa hoja kwenye kesi.[13] Walikuwa wanajadili ushahidi uliowasilishwa na wahusika wa kesi. Baadaye walikuwa wakipewa taarifa kidogo kabla ya kesi ili kujifunza ushahidi mahakamani.[13]
Matumizi nchini Wales
[hariri | hariri chanzo]Tofauti na Uskoti na Ireland ya Kaskazini, Wales si eneo la kisheria tofauti katika Ufalme wa Muungano. Sheria za zamani za Wales zilifutwa na Mfalme Henry VIII wa Uingereza kupitia Laws in Wales Acts[14]. Kuanzia 1746 hadi 1967, sheria yoyote inayotaja England ilihusisha pia Wales hadi Sheria ya Lugha ya Kiwalesi ya 1967. Sasa huitwa "Uingereza na Wales". Ingawa Wales ina uhuru wa kisiasa kiasi, haikuweza kutunga sheria hadi Sheria ya Serikali ya Wales ya 2006. Hata hivyo, mfumo wa sheria bado ni common law ya Kiingereza. Tofauti kubwa pia ni matumizi ya lugha ya Kiwalesi, ambapo sheria zake zinahusu Wales pekee. Sheria ya Lugha ya Kiwalesi ya 1993 iliweka lugha ya Kiwalesi kuwa sawa na Kiingereza kwa huduma za umma. Kiwalesi pia kinaweza kutumika mahakamani nchini Wales.
Vyanzo vya sheria ya Uingereza
[hariri | hariri chanzo]Katika Uingereza, kuna mpangilio wa vyanzo vya sheria kama ifuatavyo:
- Sheria za Umoja wa Ulaya (ubora wake ulipingwa na Brexit)
- Sheria za Bunge (kuu na za chini)
- Kanuni za kesi za common law na equity
- Mikataba ya Bunge
- Mila za kijumla
- Vitabu vya mamlaka
Kurasa zinazohusiana
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 "English Law: An introduction". In Brief. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 Piyali Syam (28 Januari 2014). "What is the Difference Between Common Law and Civil Law?". Washington University School of Law. Iliwekwa mnamo 18 Februari 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 "English Law". Duke Law School. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Percy Henry Winfield 2000. The chief sources of English legal history. Washington DC: Beard Books, p44.
- ↑ 5.0 5.1 5.2 5.3 5.4 David Robison. "The De-Evolution of Anglo-Saxon Law". Practical Law and Justice. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 18 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Weregild, pia hujulikana kama "man-price," ilikuwa ni fidia ya kifedha iliyolipwa kwa familia au ukoo wa mtu aliyeuawa au kujeruhiwa, kulingana na sheria za Anglo-Saxon England na katika sehemu nyingine za Ulaya. Katika muktadha wa common law ya Uingereza, weregild ilizingatiwa kama njia ya kusuluhisha mizozo kwa njia ya amani badala ya kulipiza kisasi au kugombana.
- ↑ 7.0 7.1 Robert Wilde. "The Consequences of the Norman Conquest". About Education. About, Inc. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Desemba 2016. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2016.
{{cite web}}
: Check|url=
value (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 8.0 8.1 8.2 8.3 8.4 "Equity Lecture Notes, Historical Introduction". LawTeacher. All Answers Ltd. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Oktoba 2016. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kwa muktadha wa kisheria, lien ni haki ya kisheria au madai ambalo mtu au shirika linaweza kuwa nalo juu ya mali ya mtu mwingine kama dhamana kwa deni au huduma iliyotolewa. Kwa maneno rahisi, lien inahakikisha kwamba mwenye deni anaweza kuweka madai juu ya mali fulani hadi deni litakapolipwa.
- ↑ "equity". Law.com/ALM. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 11.0 11.1 11.2 "Sir William Blackstone, 1723 - 1780". Online Library of Liberty. Liberty Fund, Inc. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "The Commentaries on the Laws of England". The Law Library of Queens County, 11th Judicial District, Supreme Court. New York State Unified Court System. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Juni 2010. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 13.0 13.1 13.2 "The Jury System". LawTeacher. All Answers Ltd. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Laws in Wales Acts ya 1535 na 1542 zilikuwa sheria zilizounganisha rasmi Wales na England. Zilibatilisha mifumo ya kisheria ya Wales, zikianzisha sheria za Kiingereza na kugawa Wales katika kaunti. Hii ilihakikisha uwakilishi wa Wales bungeni na kurahisisha utawala.
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sheria ya Uingereza kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |