Sharleen Spiteri (kahaba)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sharleen Spiteri alikuwa kahaba aliyeathiriwa na VVU, ambaye alifuatiliwa na vyombo vya habari, umma na serikali ya New South Wales nchini Australia baada ya kuonekana kwenye kipindi cha televisheni cha "60 Minutes (kipindi cha runinga cha Australia)" mwaka 1989, ambapo katika mahojiano aliweka wazi kwamba alikuwa akifanya mapenzi na wateja bila kuwaambia kuhusu ugonjwa wake wala kutumia kondomu.[1][2]

Baada ya kipindi cha 60 Minutes kurushwa hewani, Spiteri alishikiliwa kwa nguvu na Polisi wa New South Wales pamoja na mamlaka ya Idara ya Afya, wakitumia sehemu ya Sheria ya Afya ya Umma (Sehemu ya 32a), ambayo hapo awali ilikusudiwa kudhibiti kifua kikuu. Aliwekwa katika wadi ya UKIMWI ya Prince Henry, na kisha Hospitali ya Akili ya Rozelle kwa wiki kadhaa.

Mwanzoni mwa miaka ya 1990 kesi ya Spiteri iliendelea kuzua mjadala mkubwa wa kitaifa. Ambapo ilipelekea sheria mpya kuanziishwa huko New South Wales, inayojulikana kama "Sheria ya Sharleen" ambayo ilitaka idhini ya habari kabla ya ngono.

Japo kulikuwa na wafanyakazi wengine wa ngono katika jamii ambao pia waliathirika na VVU na kutambulika na mamlaka. Baada ya kuachiliwa, Spiteri alikuwa chini ya maagizo ya afya ya umma (pamoja na makubaliano mengine ambayo hayakuwekwa wazi na Idara ya Afya ya NSW), akitumia miaka 16 iliyobaki ya maisha yake chini ya usimamizi wa mfanyakazi wa afya wa mfumo wa Afya wa NSW kama mgonjwa. Alifariki mwaka 2005.

Mnamo mwaka 2015, Tom Morton na Eurydice Aroney, wote waandishi wa habari na wahadhiri katika Chuo Kikuu cha Teknolojia Sydney,[3][4]walichapisha Uandishi wa habari juu ya Hofu ya Maadili na Masilahi ya Umma - Kesi ya Sharleen Spiteri.[5] Jarida hilo lilihoji maadili ya kuripoti kesi ya Spiteri.[5]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "ABC Radio National Hindsight program 'Shutting Down Sharleen' (2010)". Abc.net.au. Iliwekwa mnamo 2012-05-22. 
  2. Sendziuk, Paul (1991-07-01). Learning to trust: Australian responses to AIDS By Paul Sendziuk. ISBN 9780868407180. Iliwekwa mnamo 2012-05-22. 
  3. "Tom Morton". University of Technology Sydney (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 1 May 2018.  Check date values in: |accessdate= (help)
  4. "Eurydice Aroney". University of Technology Sydney (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 1 May 2018.  Check date values in: |accessdate= (help)
  5. 5.0 5.1 Morton, Tom; Aroney, Eurydice (17 February 2015). "Journalism, Moral Panic and the Public Interest". Journalism Practice 10: 18–34. doi:10.1080/17512786.2015.1006935.  Unknown parameter |s2cid= ignored (help); Unknown parameter |hdl= ignored (help); Unknown parameter |hdl-access= ignored (help); Check date values in: |date= (help)