Shamseddin Amir-Alai
Shamseddin Amir-Alai ( 1900–Agosti 1994) alikuwa mwanasiasa wa Iran ambaye alihudumu kama Waziri wa Mambo ya Ndani na Waziri wa Sheria katika baraza la kwanza la mawaziri la Mohammad Mosaddegh. Pia, alishika nyadhifa nyingine mbalimbali za kiserikali na za kidiplomasia.
Maisha ya mapema na elimu
[hariri | hariri chanzo]Amir-Alai alizaliwa mjini Tehran mnamo mwaka 1900. Baba yake alikuwa Ali Akbar Khan Najd al Saltanah. Alitunukiwa shahada ya kwanza ya udhahiri katika fani ya fedha na utawala kutoka chuo kikuu kimoja huko Ulaya. Mnamo mwaka 1964, alipata shahada ya uzamivu (PhD) ya sayansi ya siasa mjini Paris.
Kazi na shughuli
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kurejea nchini Iran, Amir-Alai alifanya kazi katika Wizara ya Posta na baadaye katika Wizara ya Sheria.Katika wizara hiyo ya sheria, alihudumu kama jaji.[1] Baadaye, alifanya kazi katika Wizara ya Kilimo kama afisa mwandamizi.[2] Mnamo Februari 1946, aliteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo baada ya kuhudumu kama kaimu waziri katika baraza la mawaziri lililoongozwa na Waziri Mkuu Ahmad Qavam.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Pınar Arıkan Sinkaya (2015). Discursive continuity of political nationalism as a form of opposition politics in modern Iran (Tasnifu). Middle East Technical University. uk. 136. hdl:11511/25256.
- ↑ "File 11/44 Leading Personalities in Iraq, Iran & Saudi Arabia". Qatar Digital Library. 1948. Iliwekwa mnamo 16 Agosti 2023.
Citing from the British India Office Records and Private Papers
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Manshour Varasteh (Aprili 2003). Ascent and Descent of Marxist forces in Contemporary Iran Case Study: People's Fedaii & Tudeh Party (Tasnifu). University of Wales (Aberythwyth). uk. 66. CiteSeerX 10.1.1.857.3260.
{{cite thesis}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Shamseddin Amir-Alai kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |