Shalimar
Shalima Habibu ni mhusika katika tamthilia ya Siri ya Mtungi nchini Tanzania. Mhusika huyo amechezwa na Richa Adhia, ambaye ni Mtanzania. Shalima ni mwanamke kutoka Kanada. Alionekana kwa mara ya kwanza katika sehemu ya kumi na tatu ya Siri Ya Mtungi. Shalima alirudi kuchukua studio ya baba yake kutoka kwa Cheche Mtungi, mmiliki wa sasa wa biashara. Anaamini kuwa biashara hiyo ni yake, si ya Cheche. Tabia yake ni kudhibiti, kudai, kushawishi, kuwa maridadi, na kuwa na haiba. Mwishowe, alichukua biashara ya Cheche na akaigeuza kuwa ‘Shalima’s Glitz and Glamour Studio’.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Katika Siri ya Mtungi, sehemu ya kumi na tatu, Shalima aliingia kama mwanamke wa ajabu, mwenye kuvutia. Alitaka kununua petroli ya gari lake katika duka la Mzee Kizito la magari. Wafanyakazi wa duka hilo walivutiwa na Shalima, walijaza tanki la gari lake petroli, na wakasahau kumwomba Shalima alipe.
Baadaye katika utambulisho wake, aliingia studio ya Cheche, na alikataa Cheche ampige picha. Shalima alisema baba yake alimpatia Cheche studio hiyo, lakini kwa sababu yeye ni binti yake, ana haki ya biashara hiyo na studio pia. Shalima alionyesha Cheche na familia yake karatasi za Mzee Habibu kuhusu mipango ya mali na hati miliki. Zote mbili zinaonyesha kuwa biashara ya Cheche kweli ni mali ya Shalima.
Baada ya kutofautiana sana, hatimaye Cheche alikubali kuwa mshirika na Shalima baada ya kumleta wakili wake ili kuzungumza naye. Katika sehemu ya kumi na nane, Shalima alitengeneza upya studio ya Cheche Mtungi na kuiita ‘Glitz and Glamour Studio’ ya Shalima. Anataka iwe wakala wa wanamitindo badala ya studio ya picha tu. Biashara ina sura mpya ya mtindo wa kike. Analeta wanamitindo wake kama “malaika” wake, na alimwomba Cheche kuwa mpiga picha wake na kupiga picha za Shalima na wateja wake. Ingawa alisitasita, Cheche alifanya kama alivyoambiwa na kutekeleza majukumu yake. Pia, Shalima aliamua kumleta Lulu kama meneja wa studio yake, akilenga kumkosesha Cheche raha. Wawili hao wanaendelea kufanya kazi pamoja, ingawa Cheche anasitasita kukamilisha baadhi ya maombi yake, kama vile kupiga picha za wanamitindo wa uchi kwa wateja wa Shalima. Baadaye, katika Siri ya Mtungi, Cheche anagundua wosia wa awali ambao baba ya Shalima aliacha, akielezea urithi halisi wa studio ya Mzee Habibu.
Viunganishi
[hariri | hariri chanzo]Shalima ni mgeni mjini na hana marafiki wengi wa karibu. Alifanya kazi kwa ukaribu na Cheche Mtungi, lakini hawakupendana. Pia, Shalima alifanya kazi na Lulu, lakini ilionekana kuwa walikuwa washirika wa kibiashara tu
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- “Siri ya Mtungi (Episode Clip).” Youtube. https://www.youtube.com/watch?v=G8E4nXDiGPk