Serafi
Mandhari

Serafi (kwa Kiebrania: שָׂרָף, sārāf, yaani "Mwenye kuwaka"[1][2]) ni kiumbehai cha mbinguni katika dini za Uyahudi, Ukristo na Uislamu. Ingawa asili ya imani hiyo ni katika nchi ya Misri[3], Waisraeli waliipokea na kuiingiza katika ile maalumu ya kwao iliyokiri Mwenyezi Mungu kuwa mmoja tu. Aliyechangia zaidi mchakato huo ni kuhani Isaya ambaye alisimulia wito wake kama nabii kwa kueleza alivyowaona na kuwasikia maserafi wakimuimbia YHWH "Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu" (Isa 6:1-7)[4][5]. Baada yake serafi alitazamwa kama aina ya malaika.

Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ G. H. Lünemann: Imm. Joh. Gerh. Schellers lateinisch-deutsches und deutsch-lateinisches Handlexicon vornehmlich für Schulen. Zweyter oder deutsch-lateinischer Teil. Vierte verbesserte und vermehrte Auflage., Leipzig, 1820, p. 722: "Seraph, Seraphus, i, m."
- ↑ Jerrold Seigel. Between Cultures: Europe and Its Others in Five Exemplary Lives. University of Pennsylvania Press, 2015. ISBN 978-0-812-29193-3.
- ↑ Mettinger, T. N. D. (1999). "Seraphim". Katika van Der Toorn, Karel; Becking, Bob; W. Van Der Horst, Pieter (whr.). Dictionary of Deities and Demons in the Bible. Brill Publishers and W.B. Eerdmans Pub. Co. uk. 743.
...there is now an emerging consensus that the Egyptian uraeus serpent is the original source of the seraphim motif.
- ↑ Dictionary of deities and demons in the Bible. Brill. 1999. uk. 742. ISBN 978-90-04-11119-6.
- ↑ Dictionary of deities and demons in the Bible. Brill. 1999. uk. 746. ISBN 978-90-04-11119-6.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
