Semikonda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Semikonda (pia: nusukipitishi) ni aina ya kipitishi umeme chenye upitishaji ulio kati ya kipitishi halisi na kikinza.

Katika jotoridi la chini kabisa (Kelvin 0) semikonda huwa kama kikinza, lakini kadiri jotoridi linavyoongezeka, semikonda huanza kupitisha umeme kwa kuwa elektroni hupata nishati ambayo huzifanya zipande hadi kiwango cha juu cha nishati cha upitishaji.

Semikonda huwa na muundo wa viwango vya nishati za upitishi ambazo ni kiwango cha valensi, kiwango cha upitishi na kiwango tupu ambacho kipo kati ya viwango hivyo viwili.

Kuna aina mbili za semikonda, ambazo ni semikonda safi (pure semiconductor) na semikonda iliyochanganywa (impure semiconductor).

Semikonda huwa na aina mbili za visafirisha chaji ambavyo ni elektroni na mashimo. Mashimo hutokea baada ya elektroni kuondoka.

Semikonda zimekuwa muhimu sana katika teknolojia ya umemejua maana ni msingi wa seli za sola.

Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Semikonda kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.