Sehin Teferra
Mandhari
Sehin Teferra ni mwanaharakati wa haki za wanawake kutoka nchini Ethiopia[1] ambaye anahimiza dhana ya utambulisho wa Ethiopia na anajichukulia kama mfuasi wa umoja wa Ethiopia (pan-Ethiopianist).[2]
Utoto na Elimu
[hariri | hariri chanzo]Sehin Teferra alizaliwa jijini Addis Ababa. Alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Nazareth na elimu ya sekondari katika Shule ya Jumuiya ya Kiingereza ya Sanford. Alitunukiwa shahada ya awali ya masuala sosholojia katika tawi la Chuo Kikuu cha La Verne lililopo Athens, shahada ya uzamili ya maendeleo ya kimataifa akijikita katika masuala ya jinsia kutoka Chuo Kikuu cha Clark, na alihitimu shahada ya uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha SOAS jijini London mnamo mwaka 2015.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Standard4, Addis (2019-12-19), "News: Ethiopian women participation in politics up but a lot needs to be done - Addis Standard", Addis Standard (kwa American English), iliwekwa mnamo 2026-01-30
{{citation}}: CS1 maint: numeric names: authors list (link) - ↑ Martha Kuwee Kumsa (2020-12-16). "Our diverse feminists must team up to disavow epistemological violence". Ethiopia Insight (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-01-30.
- ↑ Team, AWiB, Sehin Teferra (PhD) (kwa Kiingereza (Uingereza)), iliwekwa mnamo 2026-01-30
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sehin Teferra kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |