Nenda kwa yaliyomo

Sebastien Pocognoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sébastien Jean Pocognoli (aliyezaliwa 1 Agosti 1987) ni kocha wa soka wa Ubelgiji na mchezaji wa zamani, ambaye mara ya mwisho alikuwa kocha mkuu wa klabu ya Monaco inayoshiriki Ligue 1.

Akiwa anacheza nafasi ya beki wa kushoto, Pocognoli aliwahi kuchezea klabu za Standard Liège, Genk, AZ, Hannover 96, West Bromwich Albion, Brighton & Hove Albion na Union SG.

Akiwa mchezaji wa timu za taifa za vijana za Ubelgiji kuanzia chini ya miaka 16 hadi chini ya miaka 23, alicheza jumla ya mechi 13 kwa Timu ya Taifa ya Ubelgiji.

Maisha ya Awali na Binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Pocognoli alizaliwa huko Seraing, Ubelgiji, na ana asili ya Italia.

Pocognoli alieleza kwamba baba yake alikuwa akifanya kazi karibu na uwanja wa michezo. Alipokuwa akikua, alisema kwamba mwanzoni hakupenda kabisa soka, lakini kutokana na msisitizo wa baba yake, hatimaye alianza kuipenda soka kama mchezo.[1][2]

  1. https://www.national-football-teams.com/player/27288/Sebastien_Pocognoli.html
  2. https://web.archive.org/web/20140715005658/http://www.vi.nl/nieuws/koenders-en-pocognoli-voor-vijf-jaar-naar-az.htm
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sebastien Pocognoli kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.