Sayari ya nje

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Idadi ya Sayari za Nje, kufuatana na mwaka wa kugunduliwa hadi Septemba 2014.

Sayari ya nje (ing. exoplanet, au extrasolar planet) ni sayari inayozunguka nyota isiyo Jua letu. Iko nje ya mfumo wetu.

Mnamo mwaka 2017 zaidi ya sayari za nje 3000 zinazozunguka nyota mbalimbali zilitambuliwa tayari. [1][2][3]

Kwa muda mrefu sayari nje ya mfumo wa Jua letu hazikujulikana. Giordano Bruno aliwaza mnamo karne ya 16 ya kwamba kuna dunia nyingi katika anga sawa na Dunia yetu.[4] Isaac Newton alifikiri pia ya kwamba sayari zinaweza kuwepo nje ya mfumo wetu. Lakini haikuwezakana kuthibitisha nadharia hizi.

Hadi miaka ya 1990 idadi kubwa ya wanaastronomia bado walihangaika kama sayari za nje ziko au la. Mwaka 1992 watafiti Aleksander Wolszczan na Dale Frail waliofanya kazi ya astronomia ya redio walitangaza kugunduliwa kwa sayari mbili zinazozunguka nyota tutusi (pulsar) PSR 1257+12.[5] Miaka michache baadaye taarifa hii ilithibitishwa na wagunduzi wengine.

Sizes of Kepler Planet Candidates – based on 2,740 candidates orbiting 2,036 stars as of 4 Novemba 2013 (2013 -11-04) (NASA).

Kuwepo kwa sayari ya nje inayozunguka nyota ya kawaida kulithibitishwa mara ya kwanza mwaka 1995 na watafiti wa Geneva waliogundia sayari ya nyota 51 Pegasi. Idadi iliongezeka hasa kutokana na matokeo ya utafiti wa chomboanga Kepler kilichoweza kuthibitisha kuwepo kwa mamia ya sayari za nje zenye ukubwa wa Neptun hadi Utaridi[6].

Hadi tarehe 1 Aprili 2017 jumla ya sayari za nje 3,607 zimeorodheshwa katika "Extrasolar Planets Encyclopaedia"[7]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Exoplanet Archive Planet Counts.
  2. NASA's Kepler Mission Announces a Planet Bonanza, 715 New Worlds. NASA (February 26, 2014). Iliwekwa mnamo February 26, 2014.
  3. The Habitable Exoplanets Catalog - Planetary Habitability Laboratory @ UPR Arecibo.
  4. Eli Maor (2013), uk 198
  5. Wolszczan, A.; Frail, D. A. (1992). "A planetary system around the millisecond pulsar PSR1257 + 12". Nature 355 (6356): 145–147. doi:10.1038/355145a0 .
  6. NASA's Kepler Mission Discovers 461 New Planet Candidates, tovuti ya NASA ya Jan. 11, 2013, iliangaliwa Aprili 2017
  7. Orodha ya Exoplanets, inataja " 3608 planets / 2702 planetary systems / 610 multiple planet systems", iliangaliwa Aprili 2017

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Eli Maor (1987). "Chapter 24: The New Cosmology". To Infinity and Beyond: A Cultural History of the Infinite. Springer 2013 kupitia google books hapa
Astrowiki.PNG
Mradi wa Astronomia

Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano