Nenda kwa yaliyomo

Satta Sheriff

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Satta Fatumata Sheriff ni mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Liberia, mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa Action for Justice and Human Rights(AJHR), shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi ya kudai upatikanaji wa haki na heshima kwa haki za binadamu nchini Liberia.[1][2] Yeye ni mmoja wa Vijana 100 Wenye Ushawishi Mkubwa Zaidi Afrika , kiongozi kijana wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, Umoja wa Mataifa na spika wa zamani wa Bunge la Watoto la Liberia.

Satta alizaliwa Aprili 12, 1998, wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Liberia katika kaunti ya milimani ya Bong, Wilaya ya Fulmah Bongmines; alianza elimu ya msingi akiwa na umri wa miaka sita (6).

Utetezi wa Satta ulianza akiwa na umri wa miaka (9) wakati msichana mwenzake wa miaka 13 alipotarajiwa kuolewa na mwanaume wa miaka thelathini na tisa katika jamii yake, Satta alihisi ilikuwa ni makosa; Muda mchache baadae aliongea na wazazi wa msichana huyo na kiongozi wa jamii, hivyo kusimamisha ndoa hiyo. Tangu wakati huo, amekuwa akifanya kazi kudai upatikanaji wa Haki na Heshima ya Haki za Binadamu nchini Liberia.

  1. "On Day of the African Child, Rights Groups Want Justice in Two Children's Death". The Bush Chicken. 17 June 2016. Retrieved 2018-05-18.
  2. Clay, Jackson C. (18 May 2016). "Liberia: Children Demand Justice in Rape Cases" – via AllAfrica.