Saneeya Hussain

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Saneeya Hussain (13 Agosti 1954 - 20 Aprili 2005) alikuwa mwandishi wa habari na mwanamazingira nchini Pakistani. [1] Aliolewa na mwanaume Mbrazili mwaka 1998 na alifariki nchini Brazil mwaka 2005.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Saneeya alianza kufanya kazi kama mwandishi wa makala mnamo mwaka 1978 katika MNJ nchini Pakistan.katikati ya miaka ya themanini, Saneeya alikuwa mhariri wa jarida la Star Weekend. Pia Alikua mwanachama wa Shirkat Gah Collective ambalo lilichochea Women's Action Forum, kikundi cha ushawishi ambacho kilipinga vikali utawala wa Zia. "the red scribbles " walishindwa kuvumilia, na mnamo mwaka 1988, aliondoka. Saneeya aliendelea kujiunga na World Conservation Union (IUCN)- na pia alikuwa mmoja wa Wapakistani wa kwanza kushiriki katika mawasiliano ya watu na watu na wanamazingira wa India. Pia alianzisha Kituo cha Rasilimali cha Waandishi wa Habari ambacho kiliwafunza na kuhimiza waandishi wa habari katika kuripoti kuhusu mazingira.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Saneeya Hussain week brings environment journalists together", Daily Times, 18 August 2008. Retrieved on 9 October 2013. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Saneeya Hussain kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.