Sandra "Alexandrina" Don-Arthur

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Sandra "Alexandrina" Don-Arthur

Amezaliwa 22 Aprili 1980
Ghana
Nchi Ghana
Kazi yake Msanii wa urembo na Vloga


Sandra Don-Arthur (maarufu kama Alexandrina katika tasnia ya maonesho ya biashara na urembo; alizaliwa 22 Aprili 1980) ni msanii wa urembo na Vloga (mtu anayeposti video fupi fupi kwenye mitandao ya kijamii) kutoka nchini Ghana.[1] Yeye ndiye mwanzilishi na Mkurugenzi wa Alexiglam Studio,[2] kampuni ya urembo ya Ghana inayotoa huduma za urembo kwa wanawake nchini Ghana.[1][3]

Maisha na Elimu[hariri | hariri chanzo]

Baba yake alikuwa msanifu wa majengo nchini Ghana aliyejulikana kwa jina la Dk. Eric George Alexander Don-Arthur[4][5] na mama yake alikuwa raia wa Urusi, Natalia Don-Arthur ambaye alikuwa ni mkemia. Alilelewa nchini Ghana na Urusi pamoja na kaka zake wanne na ni dada mdogo wa Eric Don-Arthur, aliyekuwa mgombea ubunge wa National Democratic Congress kwa Jimbo la Effutu mwaka 2016.[6]

Sandra alihudhuria Shule ya Morning Star huko Cantonments na kuhamia Shule ya Upili ya St. Roses katika mji wa Akwatia. Baadaye, aliondoka kwenda Uingereza kusoma Chuo cha West London na mwaka wa 2011 aliendelea na Chuo cha Mink ambako alihitimu na cheti cha ujuzi wa urembo, urembo wa nywele na athari zake. lakin pia ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Ashesi nchini Ghana.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka wa 2011, Alexandrina alianza rasmi kazi ya kuremba watu kitaaluma baada ya kumaliza kozi nchini Uingereza. Kazi yake kama msanii wa kutengeneza vipodozi ilikuja kujulikana sana wakati msanii mkuu wa urembo alipomwomba amtengenezee Mkurugenzi Mkuu wa MNET Africa, Biola Alabi kama mgeni katika kipindi cha '@ Home With…' TV Show huko jijini London.[7]

Sandra amefanya kazi na idadi kubwa ya watu mashuhuri katika tasnia ya burudani ya Ghana na Nigeria kama vile Omotola Jalade Ekehinde, Efya, Joselyn Dumas, Juliet Ibrahim, Nadia Buari, Jackie Appiah, Jim Iyke, Yvonne Okoro na DJ Cuppy.[8]

Alichaguliwa na Maybelline New York,kuwa sehemu ya sehemu ya bodi ya washawishi ili kusaidia shughuli za Maybelline nchini Ghana. Maybelline New York pia alimpa fursa ya kuwa mwenyeji wa kipindi cha kwanza cha TV cha urembo cha kwanza barani Afrika, "Makeup Diaries," ambacho kilionyeshwa kwenye DSTV katika nchi 46.[9]

Pia alikuwa mgeni na msanii mkuu wa urembo katika msimu wa kwanza wa kipindi cha "Keeping It Real" kilichoandaliwa na Mwigizaji na Mwenyeji wa Ghana, Joselyn Dumas ambapo wanawake wengi wa kisasa wa Ghana walishiriki kutoa maoni yao kuhusu mada mbalimbali zilizowaathiri mwaka wa 2017.[10] Ameunda tahariri za utengenezaji wa Jarida la Glitz Africa, Jarida la Debonair Afrika, Jarida la Harusi ya Ndoto na Jarida la Haute Canoe.[11][12]

Katika kazi yake ya urembo idadi kubwa ya viongozi wa kisiasa wa nchini Ghana pia wameguswa na mikono ya wataalamu wa Alexandrina ikiwa ni pamoja na Aliyekuwa Mke wa Rais wa Ghana, Nana Konadu Agyeman-Rawlings, Ursula Owusu, Nana Oye Lithur na aliyekuwa Mkuu wa Wafanyakazi wa kwanza wa Kike wa Ghana,[13]Frema Osei Opare na Waziri wa Mambo ya nje Shirley Ayorkor Botchway.[14]

Mnamo mwaka 2015, alihudhuria mazishi na kutoa heshima kwa marehemu Kofi Ansah kwa ushirikiano na Maybelline New York kupitia mkusanyiko huo wa Haute Avant Garde ulioangazia nguo kutoka kwa wabunifu mashuhuri wa mavazi na urembo wa nchini Ghana ili kuonyesha aina mbalimbali za bidhaa za Maybelline New York.[15]

Alichaguliwa kama msanii pekee wa kutengeneza vipodozi wa Ghana na mwakilishi wa Afrika Magharibi kushiriki katika Wiki ya Mitindo ya New York [16] na kufanya kazi na mwanamitindo Victoria Secret, Mayowa Nicholas, Sabah Koj wakati wa maonyesho ya Msimu wa baridi.[17] Mnamo 2019, alizindua lebo yake ya urembo na akademia iliyoitwa Alexiglam Studios ili kusaidia kukuza ujuzi wa urembo wa Kiafrika na kuwafunza wasanii wachanga juu ya urembo.[18]

Amehusisha ukuaji wake kama msanii wa vipodozi kutokana na tabia yake ya kudadisi alipokuwa mtoto na upendo wake wa kuvumbua mambo mapya. Pamoja na kufanya vizuri kwenye tasnia hii ya urembo hakuwa peke yake alikuwa na washauri ambao ni Pat McGrath na Bimpe Onakoya .[19]

Kazi zake zilizotambulika zaidi[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa ziara ya kifalme ya Prince Charles of Wales na mke wake Camilla, Duchess of Cornwall nchini Ghana mnamo Novemba mwaka 2018,kweye hafla iliyoandaliwa na serikali na hafla ya mini-fashion ilifanyika kwa heshima yao na Alexandrina aliteuliwa kama msanii mkuu wa urembo kwenye hafla hiyo.[20][21]Kazi yake ya uhariri kwenye uso wa mwanamitindo wa kimataifa kutoka Ghana na Nigeria, Victoria Michaels iliandikwa na kutangazwa na gazeti la Roots Magazine lenye makao yake Paris.[22]

Uhisani[hariri | hariri chanzo]

Yeye pia ni mwanzilishi mwenza wa Sickle Strong Warriors Foundation, shirika lisilo la faida ambalo linalenga kuongeza ufahamu kuhusu seli mundu na kukuza umoja miongoni mwa wagonjwa wa seli mundu nchini Ghana.[23]

Kama sehemu ya kazi zake za shirika hilo (CSR) na uhisani, pia alitumia utaalamu wake kwa mradi wa Haki Sawa, 'Nikumbuke'.[24] Ulikuwa mradi wa ushirikiano kati ya mpiga picha wa Ghana, Francis Kokoroko, Rania Odaymat, na The Fair Justice Initiative iliyolenga wanawake kumi na wawili ambao walikuwa wamehukumiwa kifungo cha maisha jela katika Magereza ya Nsawam.Kupitia mradi huo mavazi ya wanawake wa gereza yalibadilishwa na mavazi ya kitamaduni na picha zao zilipigwa ambazo zilionyeshwa katika maonyesho ya 'Make Be' huko La Maison mnamo Oktoba mwaka 2018. Tangu wakati huo kimetengenezwa kuwa kitabu cha kahawa ili kukuza utetezi.[25]

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Kwa sasa anaishi jijini Accra, Ghana na watoto wake wawili.[23]

Mwaka Tukio/Shughuli Tuzo Matokeo
2016 Tuzo za Urembo za Ghana Msanii Bora wa Uhalili wa Urembo Alishinda[26]
2018 Tuzo za Urembo za ghana Msanii Bora wa Urembo Alishinda[27]
2018 Tuzo za Wajasiriamali Vijana Ubora katika Sanaa ya Urembo Alishinda

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 https://www.myjoyonline.com/
  2. World’s leading makeup brand launches in Ghana on Friday (en-US). Citi 97.3 FM - Relevant Radio. Always (2015-04-23). Iliwekwa mnamo 2022-03-25.
  3. Sandra Don-Arthur makes Ghana proud at New York Fashion Week (en). GhanaWeb (2018-09-10). Iliwekwa mnamo 2022-03-25.
  4. Nkrumah Mausoleum decays (en). Modern Ghana. Iliwekwa mnamo 2022-03-25.
  5. An Architectural History of Ghana • The Cultural Encyclopaedia. www.culturalencyclopaedia.org. Iliwekwa mnamo 2022-03-25.
  6. Peace FM Online. Former TV3 Man Eric Don- Arthur Wins .... Peacefmonline.com - Ghana news. Iliwekwa mnamo 2022-03-25.
  7. Makeup artiste Sandra Don Arthur partners Maybelline New York (en-gb). Graphic Online. Iliwekwa mnamo 2022-03-25.
  8. ayodele johnson (2016-02-05). Actress retained as Ambassador for BO16 (en). Pulse Nigeria. Iliwekwa mnamo 2022-03-25.
  9. Top Makeup Artiste Tells Her Success Story (en). Modern Ghana. Iliwekwa mnamo 2022-03-25.
  10. https://yen.com.gh/103574-joselyn-dumas-plastic-surgery.html
  11. Frema Opare, Ursula Owusu, others cover 2017 Glitz Africa Magazine (en). GhanaWeb (2017-04-27). Iliwekwa mnamo 2022-03-25.
  12. https://www.magzter.com/GH/TOOTMAP/HAUTE-CANOE/Fashion/
  13. https://www.adomonline.com/chief-of-staff-honoured-as-model-african-woman/
  14. BellaNaija.com (2016-09-06). #WomenInspiringWomen: Glitz Africa Magazine features Ghanaian Power Women – Ursula Owusu-Ekuful, Hanna Tetteh, Nana Oye Lithur & More in the Latest issue (en-US). BellaNaija. Iliwekwa mnamo 2022-03-25.
  15. https://www.peacefmonline.com/pages/photos/1428/56627.php
  16. Sandra Don-Arthur makes Ghana proud at New York Fashion Week (en). GhanaWeb (2018-09-10). Iliwekwa mnamo 2022-03-25.
  17. Sandra Don-Arthur appears at New York Fashion Week by Sarah Taylor - Issuu (en). issuu.com. Iliwekwa mnamo 2022-03-25.
  18. Senanu Damilola Wemakor. Celebrity Make-up artist Alexandrina Don-Arthur opens studio in Ghana — Starr Fm (en-US). Iliwekwa mnamo 2022-03-25.
  19. Best of Africa, Sandra Don-Arthur (in sw-TZ), retrieved 2022-03-25 
  20. "Prince Charles in Africa: A royal visit to a land of princes and chiefs", BBC News (in en-GB), 2018-11-07, retrieved 2022-03-25 
  21. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-08-11. Iliwekwa mnamo 2022-03-25.
  22. Home (fr-FR). Roots Magazine. Iliwekwa mnamo 2022-03-25.
  23. 23.0 23.1 The telling journey of a Sickle Strong Warrior! (en-US). Citi 97.3 FM - Relevant Radio. Always (2017-06-19). Iliwekwa mnamo 2022-03-25.
  24. The Fair Justice Initiative. The Fair Justice Initiative (en-GB). The Fair Justice Initiative. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-08-11. Iliwekwa mnamo 2022-03-25.
  25. Remember Me (in sw-TZ), retrieved 2022-03-25 
  26. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-05-17. Iliwekwa mnamo 2022-03-25.
  27. Sandra Don-Arthur Wins Top Ghana Makeup Award (en). Modern Ghana. Iliwekwa mnamo 2022-03-25.