Nenda kwa yaliyomo

Salib

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kifodini cha Mt. Salib.

Salib (kwa Kiarabu: قديس صليب; kwa Kikopti: ⲫⲏⲉⲑⲟⲩⲁⲃ ⲡⲓⲥⲧⲁⲩⲣⲟⲥ; maana yake Msalaba; Mallawi, Minya, Misri, karne ya 15 - Kairo, 29 Novemba 1512) alikuwa Mkopti aliyeteswa na kuuawa na Waislamu kwa ajili ya imani yake ya Kikristo[1][2][3].

Ujanani alitamani kuishi kimonaki, lakini wazazi walimlazimisha kuoa. Hata hivyo alikubaliana na mke wake waishi kama kaka na dada[4].

Baadaye alianza kuzunguka akiwahubiria Waislamu, hivyo alifungwa na kuhukumiwa. Kwa kuwa alikataa katakata kusilimu, alisulubiwa na kutembezwa mjini juu ya ngamia hadi mwisho alikatwa kichwa[4].

Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki linamheshimu kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe aliyomfia Yesu.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. ↑ Armanios, Febe (2011). "Championing a Communal Ethos". Coptic Christianity in Ottoman Egypt. ku. 41–64. doi:10.1093/acprof:oso/9780199744848.003.0003. ISBN 978-0-19-974484-8.
  2. ↑ Armanios, Febe; Ergene, Bogac (Januari 2006). "A Christian Martyr under Mamluk Justice: The Trials of Salb (d. 1512) according to Coptic and Muslim Sources". The Muslim World. 96 (1): 115–144. doi:10.1111/j.1478-1913.2006.00120.x. INIST 17538511 ProQuest 216437990.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. ↑ "Our Relics". St. Mary and St. Shenouda's Coptic Orthodox Church (SMASS), South London. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-09-08. Iliwekwa mnamo 2025-09-10.
  4. 1 2 The Life Story Of The New Martyr Saint Pistavros. Coptic Orthodox Diocese of Mallawi. 1993. OCLC 68094567.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.