Sakramenti za uponyaji
Sakramenti za Wakatoliki na Waorthodoksi |
---|
|
Sakramenti za uponyaji, kadiri ya Kanisa Katoliki, ni sakramenti mbili zinazolenga kuponya roho na mwili wa mwamini aliyekwisha kupokea uzima mpya, wa Kimungu, katika sakramenti za kuingizwa katika Ukristo, yaani ubatizo, kipaimara na ekaristi.
Kwa kuwa uzima unaweza kuingiwa na dosari, Yesu Kristo aliweka sakramenti za kitubio na mpako wa wagonjwa ili ziponye au kurudisha uzima. Yesu alijua udhaifu wa binadamu hauishi mara anapopokea uzima wa Mungu kwa sakramenti tatu za kuingizwa katika Ukristo. Hivyo alipanga kusaidia mpaka mwisho wa dunia waamini wake watakaopatwa na dhambi na ugonjwa, kama alivyowasaidia wengi aliokutana nao katika maisha yake.
“Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, ‘Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako’... ‘Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi’ - amwambia yule mwenye kupooza - ‘Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako’. Akaondoka, akaenda zake nyumbani kwake. Makutano walipomwona, walishikwa na hofu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu amri ya namna hii” (Injili ya Mathayo 9:2,6-8).
Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki wana imani hiyohiyo, ingawa taratibu za liturujia ni tofauti.
Kumbe Waprotestanti wengi hawana ibada hizo au hawazioni kuwa sakramenti.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sakramenti za uponyaji kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |