Nenda kwa yaliyomo

Safra Catz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Safra Catz (alizaliwa Desemba 1961) ni mtendaji wa biashara nchini Marekani mwenye asili ya Israeli, makamu mwenyekiti mtendaji na aliyekuwa afisa mkuu mtendaji wa Oracle Corporation.[1] Alihamia Marekani akiwa na umri wa miaka sita na alipata shahada yake kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania na JD kutoka Chuo cha Pennsylvania Law School.[2] Alijiunga na Oracle mwaka 1999 na alikua mwenyekiti mwaka 2004.[3] Mnamo Septemba 2014, aliteuliwa kuwa afisa mkuu mtendaji mwenza pamoja na Mark Hurd, na baada ya kifo cha Hurd mwaka 2019, akawa afisa mkuu mtendaji pekee hadi Septemba 2025.[4] Mnamo Agosti 2025, utajiri wake ulikadiriwa kuwa dola bilioni 3.1.[5]

  1. "Safra A. Catz | Executive Biography". Oracle.com.
  2. Rochelle Garner (December 19, 2006). "Heir apparent at Oracle is credited with growth strategy". International Herald Tribune.
  3. Oracle Co-President Safra Catz Adds CFO Duties as Jeff Epstein Leaves, allthingsd.com, April 25, 2011.
  4. Grant, Nico (December 12, 2019). "Safra Catz to Remain Sole Oracle CEO After Mark Hurd's Death". Fortune.
  5. "Safra Catz". Forbes.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Safra Catz kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.