Nenda kwa yaliyomo

Saffron Aldridge

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Saffron Aldridge (alizaliwa 1968) ni mwanaharakati, mwandishi wa habari, na mwanamitindo kutoka Uingereza. Akiwa na umri wa miaka kumi na sita, alipata umaarufu akiwa anafanya kazi kwa Ralph Lauren katika miaka ya 1990.[1] Ndugu zake ni pamoja na mpiga picha wa mitindo anayeitwa Miles Aldridge[2] na dada zake wa kambo Lily Aldridge na Ruby Aldridge ni wanamitindo.

Maisha ya Awali

[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa eneo la Parliament Hill, kaskazini mwa jiji la London. Wazazi wake Saffron ni Alan Aldridge na Rita Farthing. Kuanzia umri wa miaka 13 hadi 16, alifanya kazi katika soko la Camden Lock. Alimfahamu msichana aliyefanya kazi kwenye kibanda ambaye alikuwa pamoja na wakala wa uanamitindo wa Take Two, ndipo siku moja aliamua kwenda pamoja naye na wakamchukua rasmi.[3]

Aldridge alianza  uanamitindo akiwa na umri wa miaka kumi na sita akivaa vito vya mapambo kwa ajili ya jarida linaloitwa Uwanja.[4]

Akiwa na umri wa miaka 17, alipata bahati ya kushiriki katika kampeni ya Ralph Lauren kama mtu wa nyongeza kwa sababu rafiki yake alimjua Bruce Weber, ambaye alikuwa akipiga kampeni hiyo. Kutokana na hivyo aliweza kupewa mkataba wake wa kwanza na Ralph na kuanzia hapo, Aldridge alipata umaarufu kama sura ya zamani ya Ralph Lauren.[3]

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya wazazi wake kupeana talaka akiwa na umri wa miaka minane, Aldridge aliishi pamoja na mama yake na kaka zake Marc na Miles Aldridge, Kaskazini mwa London.[5] Wanamitindo Lily na Ruby Aldridge ni dada zake wa kambo kutoka ndoa ya pili ya Alan huko Los Angeles.[6]

  1. "Saffron Aldridge", Tatler (kwa Kiingereza), ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-07-07, iliwekwa mnamo 2026-01-30
  2. "Miles Aldridge - Vogue.it". www.vogue.it. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-09-26. Iliwekwa mnamo 2026-01-30.
  3. 1 2 "The secret of my success: Saffron Aldridge". The Independent (kwa Kiingereza). 1998-09-26. Iliwekwa mnamo 2026-01-30.
  4. Morag Preston, Evening Standard (2012-04-13). "Model behaviour". The Standard (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-01-30.
  5. Sweeting, Adam (2017-02-22), "Alan Aldridge obituary", The Guardian (kwa Kiingereza (Uingereza)), ISSN 0261-3077, iliwekwa mnamo 2026-01-30
  6. Tatler (2013-04-22). "Lily Aldridge: Red hot mama". Tatler (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2026-01-30.