Sabrina Carpenter
| Sabrina Carpenter | |
|---|---|
| Amezaliwa | Sabrina Annlynn Carpenter Mei11, 1999 (miaka 27) Quakertown, Pennsylvania, Marekani |
| Kazi yake | Muimbaji, Mtunzi wa nyimbo, muigizaji |
| Miaka ya kazi | 2008-sasa |
| Mtindo | Pop, R&B |
| Saini | |
Sabrina Annlynn Carpenter (alizaliwa 11 Mei 1999) ni mwimbaji, mwandishi wa nyimbo, na muigizaji wa Marekani. Tuzo alizowahi kutunukiwa ni pamoja na Tuzo mbili za Grammy, Tuzo moja ya Emmy, Tuzo tatu za American Music Awards, Tuzo moja ya Brit Award, na Tuzo sita za MTV Video Music Awards. Alitambuliwa na jarida la Time kwenye orodha yao ya Time 100 Next mnamo mwaka 2024. Carpenter alipata umaarufu mkubwa kwa kuigiza kama Maya Hart kwenye safu ya vipindi vya Disney Channel ya Girl Meets World (2014–2017). Alisaini mkataba na kampuni ya Hollywood Records na kupata mafanikio ya kiasi tu na albamu zake za studio za Eyes Wide Open (2015), Evolution (2016), Singular: Act I (2018), na Singular: Act II (2019).[1][2]
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Sabrina Annlynn Carpenter alizaliwa mnamo Mei 11, 1999, huko Quakertown, Pennsylvania, kwa wazazi David na Elizabeth (jina la utotoni Sneidar) Carpenter, na alilelewa huko East Greenville.[3] Dada yake mkubwa zaidi, Shannon, ni mnenguaji (dancer). Dada yake mkubwa, Sarah, ni mshirika wake katika kazi za ubunifu na ni mpiga picha[4]. Pia wana dada mkubwa wa kambo upande wa baba yao anayeitwa Cayla, ambaye ni msusi na mtaalamu wa urembo (makeup artist). Baba yao ni kaka wa kambo wa muigizaji Nancy Cartwright. [5]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Oktoba 2008, Carpenter alikuwa mmoja wa washiriki 7,000 walioingia kwenye shindano la mtandaoni la uimbaji la The Next Miley Cyrus Project, ambalo liliendeshwa na Miley Cyrus. Alishika nafasi ya tatu mnamo mwaka 2010. Karibu na kipindi hicho, Carpenter alisaini mkataba na meneja Bill Perlman.[6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://web.archive.org/web/20171110225320/https://ohmy.disney.com/music/2014/10/13/sabrina-carpenter-takes-the-playlist-pop-quiz/
- ↑ https://virginradio.co.uk/music/146708/why-are-people-arguing-about-sabrina-carpenters-espresso-lyrics-what-is-the-debate-about-the-comma-what-does-the-song-mean
- ↑ https://people.com/all-about-sabrina-carpenter-parents-elizabeth-and-david-carpenter-8584964
- ↑ https://people.com/all-about-sabrina-carpenter-siblings-8598810
- ↑ https://www.biography.com/musicians/a62488913/sabrina-carpenter
- ↑ https://people.com/sabrina-carpenter-opens-up-about-working-with-her-sister-sarah-11945142
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sabrina Carpenter kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |