Saara Kuugongelwa
Mandhari
Saara Kuugongelwa-Amadhila (amezaliwa 12 Oktoba 1967) ni mwanasiasa wa Namibia anayehudumu kama Spika wa Bunge la Taifa la Namibia tangu tarehe 21 Machi 2025. Alihudumu kama Waziri Mkuu wa Namibia kuanzia mwaka 2015 hadi 2025. Ni mwanachama wa South West Africa People's Organization (SWAPO) na amekuwa mbunge wa Bunge la Taifa la Namibia tangu mwaka 1995. Pia aliwahi kuwa Waziri wa Fedha kuanzia mwaka 2003 hadi 2015.[1] Pia ni mwanamke wa kwanza kuhudumu kama Waziri Mkuu wa Namibia.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Kuugongelwa-Amadhila, Saara". Namibian Parliament (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-02-24.
| Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Saara Kuugongelwa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |