Saalumarada Thimmakka
Saalumarada Thimmakka, vile vile anajulikana kama Aala Marada Thimmakka, ni mwanamazingira wa Uhindi kutoka jimbo la Karnataka, anayejulikana kwa kazi yake ya kupanda na kutunza miti 385 aina YA banyan (Ficus benghalensis) kwenye eneo linalochukua takribani kilomita arobaini na tano kufuata barabara kuu kati ya Hulikal na Kudur. Pia amepanda karibu miti mingine 8000. [1] Haya yote alifanikiwa kwa kushirikiana na mume wake.
Mwanzo hakubahatika kupata elimu rasmi, alifanya kazi kama mfanyakazi wa kawaida katika machimbo ya mawe ya jirani. [2] Kazi yake ilitambuliwa na Serikali ya India nakupewa tuzo ya heshima ya raia wa India ya Padma Shri mnamo 2019.
Shirika la mazingira la Marekani lililoko Los Angeles na Oakland, California liitwalo Rasilimali za Thimmakka kwa Elimu ya Mazingira (en. Thimmakka's Resources for Environmental Education) lilipewa jina lake. [3] Mnamo mwaka 2020 Chuo Kikuu cha Kati cha Karnataka (Eng. Central University of Karnataka) kimetangaza udaktari wa heshima wa Thimmakka [4].
Maisha ya zamani
[hariri | hariri chanzo]Thimmakka alizaliwa huko Gubbi Taluk, Wilaya ya Tumukuru huko Karnataka. Aliolewa na Chikkaiah, mzaliwa wa kijiji cha Hulikal huko Magadi taluk ya wilaya ya Ramanagara huko Karnataka . Wenzi hao hawakuweza kupata watoto lakini, walikuwa wameasili mtoto wa kiume anayeitwa Surya Prakash. Inasemekana kwamba Thimmakka alianza kupanda miti ya banyan badala ya watoto. Jina la Saalumarada ( safu ya miti katika lugha ya Kikannada ) ndivyo alivyorejelewa kwa sababu ya kazi yake.
Miti ya Ficus (banyan) ilikuwa mingi karibu na kijiji cha Thimmakka. Hivyo Thimakka na mumewe walianza kupandikiza miche kutoka kwenye miti hii iliyokuwa imeota kijiji kwao kama mbegu. Walifanikiwa kupandikiza miche kumi na kuipanda kwa umbali wa kilometa 5 kila mtu kwa mwaka wa kwanza, kisha wakapandikiza miche 15 kwa mwaka wa pili, na baadae niche 20 kwa mwaka wa 3, Yote haya walifanikiwa kwakutumia rasilimari duni walizokuwa nazo. Hawakuishia hapo wawili hawa walilazimika kutembea umbari wa kilometa 4 wakiwa na ndoo za maji kichwani hasa kwakipindi cha kiangazi kwaajili ya kumwagilia miti waliyoipanda. vile vile waliiwekea uzio miti waliyo ipanda ili kuikinga na uharibifu hasa wa wanyama kama ng'ombe .
Miche hiyo ilipandwa zaidi wakati wa msimu wa masika ili maji ya mvua ya kutosha yawepo. Kufikia mwanzo wa misimu ya kipupwe iliyofuata, miche ilikuwa imeota mizizi. Kwa jumla, miti 384 ilipandwa, na thamani ya mali yake imekadiriwa kuwa karibu rupia milioni 1.5. [5] Usimamizi wa miti hii sasa umechukuliwa na Serikali ya Karnataka . [6]
Kwa mafanikio yake, Thimmakka ametunukiwa tuzo na nukuu zifuatazo:
- Tuzo la Padma Shri - 2019
- Tuzo la Nadoja Na Chuo Kikuu cha Hampi - 2010
- Tuzo ya Raia wa Kitaifa - 1995 [7]
- Tuzo za Indira Priyadarshini Vrikshamitra - 1997 [7]
- Tuzo la Veerachakra Prashasthi - 1997
- Cheti cha Heshima kutoka Idara ya Ustawi wa Wanawake na Watoto, Serikali ya Karnataka
- Cheti cha Shukrani kutoka Taasisi ya India ya Sayansi ya Mbao na Teknolojia, Bangalore .
- Tuzo la Karnataka Kalpavalli - 2000
- Godfrey Phillips Tuzo la Ushujaa - 2006. [8]
- Tuzo la Vishalakshi na Sanaa ya Shirika Hai
- Tuzo ya Vishwathma na Hoovinahole Archived 18 Mei 2021 at the Wayback Machine. Foundation -2015
- Mmoja wa Wanawake 100 wa BBC katika 2016 [9]
- Imeheshimiwa kwa Tuzo la She's Divine na I and You Being Together Foundation 2017
- tuzo ya Parisara Rathana
- tuzo ya bingwa wa kijani
- tuzo ya Vriksmatha
Mnamo 2016, Saalumarada Thimmakka aliorodheshwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza kama mmoja wa wanawake wenye ushawishi na msukumo zaidi ulimwenguni.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ PTI. "Watch: When The "Mother Of Trees" Blessed President Ram Nath Kovind", NDTV.com, 16 March 2019.
- ↑ "The 300 trees of Thimmakka and Chikkanna". www.goodnewsindia.com. Iliwekwa mnamo 14 Februari 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "About Thimmakka". Online Webpage of Thimmakka.org. Thimmakka's Resources for Environmental Education. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 31 Desemba 2006. Iliwekwa mnamo 23 Mei 2007.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "ಕೇಂದ್ರೀಯ ವಿಶ್ವವಿದ್ಯಾಲಯದಿಂದ ಸಾಲುಮರದ ತಿಮ್ಮಕ್ಕ ಸೇರಿ ಐವರಿಗೆ ಗೌರವ ಡಾಕ್ಟರೇಟ್".
- ↑ A biography of Thimmakka is provided by B. R. Srikanth. "Thimmakka's Green Crusade Transforms Heat-And-Dust Hulikal". Online Edition of The Outlook, dated 1999-05-03. © Outlook Publishing (India) Private Limited. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 18 Februari 2008. Iliwekwa mnamo 23 Mei 2007.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)B. R. Srikanth. - ↑ Thimmakka started to plant banyan trees to overcome the grief of being childless: Priyanjana Dutta. "Woman plants trees, village thrives". Online webpage of Ibnlive.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-30. Iliwekwa mnamo 23 Mei 2007.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)Priyanjana Dutta. - ↑ 7.0 7.1 Planting of tree by Thimmakka and the Chikkaiah is mentioned by Malini Shankat. "A mother's love". Online webpage of DownToEarth.org. ©2004 Society for Environmental Communications. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Septemba 2007. Iliwekwa mnamo 23 Mei 2007.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)Malini Shankat. - ↑ "Unsung heroes' hour of glory", The Hindu. Retrieved on 2022-04-20. Archived from the original on 2007-08-09.
- ↑ 2016, BBC, Retrieved 26 November 2016