S2Kizzy
Salmin Kasimu Maengo (maarufu kwa jina lake la kisanii S2KIZZY, amezaliwa 9 Mei 1996) ni mtayarishaji wa muziki na mtunzi wa nyimbo kutoka Tanzania. Anafahamika zaidi kwa kutengeneza nyimbo za Bongo Flava “Amaboko” na “Tetema” za Rayvanny akimshirikisha Diamond platnumz. Ametayarisha albamu na kusimamia kazi za Diamond Platnumz, Rayvanny, Bill Nass na Vanessa Mdee. Anasifiwa kuwa 'mtayarishaji bora' katika muziki wa kisasa wa Bongo-Flava, Bongo-Trap, Afrobeats na Afro-pop.[1]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Maengo ndiye mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Pluto Records, lakini anafanya kazi hasa na WCB (Wasafi Classic Baby).[2]
Huenda Amber Rose anafanya naye kazi kwenye mradi. [3]
Maisha ya awali na mwanzo wa kazi
[hariri | hariri chanzo]Salmin, aliyepewa jina la Rais wa Zanzibar Marehemu Salmin Amour, alizaliwa Mbeya, na kulelewa na shangazi yake kama wake. Mama yake alifariki akiwa na umri wa miaka 3, muda mfupi baada ya hapo baba yake aliondoka na kuoa tena. Alilelewa katika maadili ya Kiislamu.
Shauku yake ya muziki ilianza mapema, na akiwa shule ya msingi alianza kujifunza jinsi ya kupiga ngoma. Baadaye, akiwa sekondari alisoma shule ya bweni ya kwiro boys iliyopo Morogoro, Tanzania.
Marèjeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "7 Bongo-Trap Songs You Need to Hear Right Now | OkayAfrica". www.okayafrica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-08-22.
- ↑ Charles Maganga (2019-05-27). "WEUSI - Showtime". NotjustOk (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-08-22.
- ↑ CLOUDSMEDIA (2020-12-16), s2KIZZY na AMBER ROSE"Nini kinaendelea"/ baba ALIYEMBAKA mtoto wake"JELA kifungo cha maisha...!", iliwekwa mnamo 2025-08-22