Runinga ya rununu
Runinga ya rununu ni runinga inayotazamwa kwa kifaa kidogo cha kubebwa mkononi au kifaa mpakato, ambacho hutengenezwa kwa madhumuni hayo. Inajumuisha huduma inayotolewa kupitia mitandao ya simu za mkononi, inayorushwa hewani bure kupitia vituo vya televisheni, au kupitia matangazo ya satelaiti. Viwango vya kawaida vya utangazaji au fomati maalum za utangazaji za rununu zinaweza kutumika. Vipengele vya ziada ni pamoja na kupakua programu za Televisheni na podikasti kutoka kwa Mtandao na kuhifadhi programu kwa ajili ya kutazamwa baadaye.
Kulingana na Harvard Business Review, kuongezeka kwa matumizi ya simu janja kumeruhusu watumiaji kutazama video nyingi za rununu katika siku tatu za Olimpiki ya Majira ya Baridi ya 2010 zaidi ya walivyotazama katika Michezo yote ya Olimpiki ya Majira ya Joto 2008, ikiwa ni ongezeko la mara tano.[1] Hata hivyo isipokuwa Korea Kusini, kukubalika kwa watumiaji wa matangazo ya runinga ya rununu kumepunguzwa kwa sababu ya ukosefu wa vifaa vinavyotangamana.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 4 Ways Smartphones Save TV TV Genius Blog. 31 January 2011. Archived 30 Aprili 2011 at the Wayback Machine
- ↑ Winslow, George (23 Aprili 2012). "Mobilizing for Mobile DTV". Broadcasting & Cable. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Desemba 2012. Iliwekwa mnamo 29 Juni 2012.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |