Rungwe (mlima)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mlima wa Rungwe katika Nyanda za Juu za Kusini za Tanzania

Mlima wa Rungwe ni volkeno iliyozimika ya Tanzania kusini magharibi ikikadiriwa ya kwamba mlipuko wake wa mwisho ulitokea mnamo miaka 2000 hadi 5000 iliyopita. Ukiwa na kimo cha 2960 m ni mlima mkubwa wa Tanzania ya Kusini.

Mlima unasimama juu ya ncha ya kaskazini ya Ziwa Nyasa. Upande wa kusini-mashariki wa mlima hupokea usimbishaji wa 3,000 mm kwa mwaka ambao ni juu kabisa katika Tanzania.

Mazingira ya mlima ni nchi yenye rutba na kilimo. Rungwe ni eneo la Wanyakyusa.

Jina la mlima limekuwa pia jina la wilaya ya Rungwe.]