Nenda kwa yaliyomo

Ruhila Adatia-Sood

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ruhila Adatia-Sood

Ruhila Adatia-Sood (29 Agosti 1982 - 21 Septemba 2013) mwenye asili ya India alikuwa mwandishi wa habari na alitangaza kwa Televisheni na Radio nchini Kenya .

Ruhila Adatia alizaliwa na kulelewa Kisumu na jijini Nairobi. [1] Alihitimu masomo ya msingi katika shule ya Aga Khan Academy jijini Nairobi na mwaka wa 2007akahitimu kutoka chuo kikuu cha Rhodes kilichoko Grahamstown Afrika Kusini.Baada ya kuhitimu mwaka wa 2007, alifanya kazi nchini Kenya katika vyombo vya habari tofauti ikiwemo Radio Africa Group kama msomaji wa habari, msimamizi wa kipindi cha Rankingshow katika radio ya Kiss 100 na Metro East FM,kituo cha radio kinacholenga jamii ya Wahindi nchini Kenya.Kuanzia mwaka wa 2011 walikuwa na kipindi cha Televisheni cha watoto kupika walichokuwa wakirekodi kila mwezi katika jumba la maduka la Westgate jijini Nairobi wakiwa na msimamizi wa kipindi hicho Kamal Kaur.

Alikuwa mwanachama wa jamii ya Kiislamu ya Ismaili.Mwezi wa January mwaka wa 2012, aliolewa na Ketan Sood mwanachama wa shirika la USAID jijini Nairobi. Harusi ilifanyika katika Hekalu ya Arya Samaj ilioko eneo la Parklands jijini Nairobi.

Ruhila alijeruhiwa katika kisa cha ufyatuaji risasi katika jumba hilo la maduka la Westgate alipokuwa akiandaa mashindano ya kupika ya watoto katika paa la jumba hilo. Aliaga dunia njiani akikimbizwa katika hospitali ya Aga Khan kwa matibabu. Wakati wa kifo chake akiwa na umri wa miaka 31, alikuwa na mimba ya kati ya miezi sita na saba ya mtoto wake wa kwanza.

  1. Mukel, Catherine (15 Septemba 2012). "Kenya: Relative Values - I Had My First Relationship in My 20s, It Was Approved By My Sisters and Friends". The Star. Iliwekwa mnamo 23 Septemba 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ruhila Adatia-Sood kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.