Rugiatu Turay

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Rugiatu Turay ni mwanaharakati wa haki za wanawake raia wa Sierra Leone.[1] Turay ni mwanaharakati mwenye msimamo mkali dhidi ya ukeketaji wa wanawake. [2] Ni mwanzilishi wa The Amazonian Initiative Movement, shirika lisilo la faida lenye malengo ya kutokomeza ukeketaji katika Afrika Magharibi.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Turay alipokuwa na umri wa miaka 11, yeye, pamoja na [[[dada]] zake, walipaswa kumtembelea shangazi yao katika mji mkuu wa nchi hiyo, Freetown.[3] Walipofika tu, Turay alifungwa kitambaa usoni kwa nguvu na kulazwa chini kisha wanawake wakamkalia kifuani, kwenye mikono na miguu. Kitambaa kikasokomezwa mdomoni mwake na kuvuliwa nguo. huku wanawake wakipiga makofi, kuimba, na kupaza sauti kuwa siku hiyo amekuwa mwanamke rasmi/kamili. Kilichotekea ni kwamba hakuwa amepelekwa kumtembelea shangazi yake bali kukeketwa. Mwanamke mmoja alitumia kisu butu kukata sehemu zake za siri. Wanawake wengine walimuonya asije akasema chochote kuhusu tukio hilo la sivyo atakufa.[4]

Turay anakumbuka kwamba kitendo kile kilikuwa cha maumivu makali sana na pia aliendelea kuvuja damu kwa siku mbili mfululizo. Anakumbuka alizimia pale alipojaribu kutembea. Kidonda kilipopona, kovu lilikuwa linawasha na kupata maambukizi. Kwa sababu hii, alikuwa anapata maumivu makali sana wakati wa hedhi na ilisababisha damu kuganda (blood clots) na kupata uvimbe.[3]

Ilipofika zamu ya mdogo wake Turay kukeketwa, Turay alijaribu kuingilia kati, lakini hakufanikiwa. Binamu yake alipofariki kwa sababu ya mila hizi, alipata nguvu ya kuanzisha kampeni ya kupinga ukeketaji huu.[3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. TERRE DES FEMMES - Menschenrechte für die Frau e.V. - Sierra Leone (de-de). TERRE DES FEMMES. Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-12-04. Iliwekwa mnamo 2 September 2020.
  2. "5 Activists Leading the Fight Against Female Genital Mutilation in Africa", Global Citizen, Global Citizen, 5 February 2020. Retrieved on 2 September 2020. (en) 
  3. 3.0 3.1 3.2 "WHO | Fighting genital mutilation in Sierra Leone", WHO, World Health Organization. Retrieved on 2 September 2020. 
  4. Rugiatu Turay – www.gocampaign.org. GO Campaign. Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-09-30. Iliwekwa mnamo 2 September 2020.
People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rugiatu Turay kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.