Rudo Chakwera
Rudo Chakwera (amezaliwa 23 Desemba 1979) ni mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Malawi. Ni mkwe wa Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera.
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa na Isaac Mkukupa na Gloria Rose Mkukupa, familia yenye asili ya muziki. Ameolewa na Nick Chakwera na wana watoto watatu.
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Rudo ana shahada ya kwanza ya muziki kutoka Chancellor College ya University of Malawi, na pia ana shahada ya uzamili katika utawala wa biashara (MBA) kutoka ESAMI.[1]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Ingawa alianza kuimba tangu utotoni, alipata umaarufu katika tasnia ya muziki nchini Malawi mwaka 1999 kupitia albamu yake ya kwanza iliyokuwa na wimbo Ndine Mwana Wamasiye.[2]
Rudo ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya kitaifa ya chama cha wanamuziki nchini Malawi. Pia amewahi kuhudumu kama mjumbe wa bodi ya Copyright Society of Malawi na bodi ya kituo cha redio cha Channel for All Nations.[3]
Mwaka 2022, katika siku yake ya kuzaliwa, alitembelea Maula Prison mjini Lilongwe na kuwaburudisha vijana waliokuwa gerezani hapo pamoja na wanamuziki wengine akiwemo Chikondi Wiseman. Kituo hicho cha vijana wahalifu kilikuwa kipya na kilikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa chakula.[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "bridgeAFRIC Signs Malawian gospel Artiste, Rudo Chakwera". This Day. Iliwekwa mnamo Julai 31, 2024.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Abiodun, Alao (16 Julai 2024). "BridgeAFRIC signs Malawian gospel artiste Rudo Chakwera". The Nation. Lagos, Nigeria. Iliwekwa mnamo 31 Julai 2024.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "BridgeAFRIC signs Malawian gospel artiste Rudo Chakwera;set to release new project". Vanguard. Lagos, Nigeria. 15 Julai 2024. Iliwekwa mnamo 31 Julai 2024.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kalumbi, Mike (2022-12-25). "Musician Rudo celebrates with young offenders at Maula Prison". Malawi 24 (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2026-03-26.
| Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Rudo Chakwera kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |