Ronke Ademiluyi
Mandhari
| Her Royal Majesty Olori Aderonke Ademiluyi-Ogunwusi | |
|---|---|
| | |
| Jina la kuzaliwa | Ronke Ademiluyi |
| Nchi | Nigeria |
| Kazi yake | Mfanyabiashara |
| Ndoa | Ameolewa |
Malkia Ronke Ademiluyi-Ogunwusi ni mjasiriamali wa mitindo kutoka Nigeria. Yeye ni Olori (Malkia) wa Ufalme wa Ife mwenye uraia wa Uingereza na Nigeria, aliyezaliwa katika ukoo wa kifalme. Ni mjukuu wa kizazi cha nne wa marehemu Ooni Ajagun Ademiluyi, Mfalme wa 48 wa Ufalme wa Ile-Ife uliopo Kusini Magharibi mwa Nigeria. Ameolewa na Ooni Adeyeye Enitan Ogunwusi, ambaye ni Ooni wa 51 wa Ife.
Mheshimiwa Malkia Aderonke Ademiluyi-Ogunwusi ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha London, alikohitimu masomo ya Sheria. Mwaka 2011 alianzisha jukwaa la kimataifa la mitindo lijulikanalo kama Africa Fashion Week London.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Alfred, Kayode (30 Juni 2016). "Nigeria: Africa Fashion Week Nigeria Takes Off". Vanguard News. Iliwekwa mnamo 18 Julai 2016.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ronke Ademiluyi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |