Roland Emmerich
Roland Emmerich | |
---|---|
Roland Emmerich mjini Berlin (2007) | |
Amezaliwa | 10 Novemba 1955 Stuttgart, Baden-Württemberg, West Germany |
Kazi yake | Mwongozaji wa filamu, mtayarishaji na mwandishi-skrini |
Miaka ya kazi | 1984–mpaka sasa |
Roland Emmerich (amezaliwa 10 Novemba 1955) ni mwongozaji wa filamu, mwandishi-skrini, na mtayarishaji kutoka nchini Ujerumani. Anafahamika sana kwa kutengeneza filamu nyingi za majanga na mapigano. Filamu zake zimepata jumla ya mauzo zaidi ya $ bilioni 3 kwa hesabu ya dunia nzima, na kuwa zaidi ya hao wazawa wengine-waongozaji filamu kutoka barani Ulaya. Filamu zake zimepata mapato zaidi ya bilioni $1 kwa nchini Marekani, na kumfanya kuwa mwongozaji filamu wa nchini humo wa 14 kwa mapato makubwa wa muda wote.[1][2][3] Ameanza shughuri zake katika soko la filamu kwa kuongoza filamu ya The Noah's Ark Principle ikiwa kama moja ya tasnifu yake akiwa Chuo Kikuu na kuwa mmoja kati walioanzisha kampuni ya utengenezaji wa filamu ya Centropolis Film Productions mnamo 1985 akiwa na dada'ke. Vilevile anafahimika kwa kuweka bayana kuwa yeye ni bwabwa.
Maisha ya awali na kazi
[hariri | hariri chanzo]Emmerich alizaliwa mjini Stuttgart, Ujerumani na kukulia katika kitongoji cha Sindelfingen.[4] Akiwa kijana, amepata kusafiri mbali kabisa huko barani Ulaya na Amerika ya Kaskazini katika matembezi yaliyotolewa hela na baba'ke, Hans, tajiri mwanzilishi wa kampuni ya utengenezaji wa mashine za bustani.[5] Mnamo mwaka wa 1977, akaanza kusoma katika Chuo Kikuu cha Filamu na Televisheni cha Munich akiwa na nia ya kusomea msanifu matayarisho. Baada ya kutazama Star Wars Episode IV: A New Hope, akaamua kujiandikisha katika shule za vipindi vya uongozaji wa filamu.[6] Akatengeneza kipande kifupi cha filamu kikiwa kama hitimisho la tasnifu yake mnamo mwaka wa 1981, ametunga na kuongoza urefu mzima wa The Noah's Ark Principle, ambayo hatimaye ilichaguliwa kama filamu funguzi ya Tamasha la Filamu la Berlin la mwaka wa 1984.[7]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Roland Emmerich". boxofficemojo.com. Iliwekwa mnamo 2009-03-16.
- ↑ "Roland Emmerich". the-numbers.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-04-11. Iliwekwa mnamo 2009-03-16.
- ↑ "The top 25 highest grossing film directors". The New Politickler. 16 Januari 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-10-16. Iliwekwa mnamo 2009-03-16.
- ↑ Rebecca Ascher-Walsh. "Space Under Fire", Entertainment Weekly, 22 Agosti 1995. Retrieved on 2008-07-08. Archived from the original on 2011-08-16.
- ↑ By Hilary Whiteman. "Roland Emmerich, the accidental director openly gay", CNN, 7 Machi 2008. Retrieved on 2009-03-16.
- ↑ The Force Is With Them: The Legacy of Star Wars Star Wars Original Trilogy DVD Box Set: Bonus Materials, [2004]
- ↑ By Hilary Whiteman. "Roland Emmerich: Making it big", CNN, 10 Machi 2008. Retrieved on 2009-03-16.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Roland Emmerich at the Internet Movie Database
- Roland Emmerich Producer Profile for The 1 Second Film Archived 25 Agosti 2009 at the Wayback Machine.
- Interview with Roland Emmerich from July 2009
- Centropolis Entertainment Archived 29 Agosti 2018 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Roland Emmerich kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |