Rodolfo Pio da Carpi
Mandhari
Rodolfo Pio da Carpi (22 Februari 1500 – 2 Mei 1564) alikuwa askofu, kardinali, mwanahistoria, na mtetezi wa sanaa wa Italia.
Alikuwa mtoto wa ndugu wa mwanadiplomasia Alberto Pio da Carpi, ambaye alifundishwa na Pico della Mirandola na alikuwa mwanafalsafa maarufu. Mwenyewe akawa mwanadiplomasia afikapo umri wa miaka thelathini, akijulikana na Kaizari Karoli V na Mfalme Francis wa Ufaransa, na alifanya mazungumzo na wote wawili kwa niaba ya Papa.[1]
Ushirikiano na Alberto ulikuwa msingi wa malezi na elimu ya Rodolfo. Aliunda maktaba maarufu na kushiriki katika masomo ya wanahistoria wa karne ya 16 mjini Roma; pia alihudumu katika Mahakama ya Kuchunguza Uzushi. Alisaidia kuanzisha mahakama hiyo huko Milano.[2]

Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Pio, Giovanni Michele (1615). Della Nobile et generosa progenie del P. S. Domenico in Italia libri due (kwa Italian). Bologna: B. Cochi. uk. 280.
{{cite book}}: CS1 maint: unrecognized language (link) His colleagues as supremi giudici nel Tribunale del Sancto Officio were: Cardinals Giovanni Pietro Carafa (Pope Paul IV, 1555–1559), Marcello Cervini (Pope Marcellus II, 1555), and F. Giovanni of Toledo. - ↑ Hoffmann, Christiane (1989). Kardinal Rodolfo Pio da Carpi und seine Reform der Aegidianischen Konstitutionen. Berlin: Duncker & Humblot. uk. 11. ISBN 978-3-428-46708-2.
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |