Nenda kwa yaliyomo

Robin Gosens

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Robin Gosens

Robin Everardus Gosens (aliyezaliwa 5 Julai 1994) ni mchezaji wa kulipwa wa mpira wa miguu wa Ujerumani anayocheza katika nafasi ya beki wa kushoto au wing-back wa kushoto.

Kwa sasa anachezea klabu ya Schalke 04 ya Bundesliga kwa mkopo kutoka klabu ya Fiorentina ya Serie A, pamoja na timu ya taifa ya Ujerumani.

Maisha ya Klabu

[hariri | hariri chanzo]

Gosens alizaliwa Emmerich am Rhein, Ujerumani. Alianza kucheza katika klabu za eneo hilo kama Fortuna Elten, 1. FC Bocholt na VfL Rhede, kabla ya kujiunga na mfumo wa vijana wa Vitesse tarehe 4 Julai 2012.

Tarehe 13 Agosti 2013, alisaini mkataba wake wa kwanza wa kulipwa na klabu hiyo.

Kabla ya hapo, Gosens alishindwa kufaulu katika majaribio ya kujiunga na Borussia Dortmund, moja ya klabu kubwa za Bundesliga. Gosens mwenyewe alielezea jaribio hilo kuwa “janga”.[1][2]

  1. https://datencenter.dfb.de/en/data-center/people/robin-gosens/player
  2. https://web.archive.org/web/20210505214243/https://www.atalanta.it/en/grow-characters/robin-gosens/
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Robin Gosens kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.