Rita Ora
| Rita Ora | |
Ora mjini Berlin, 2018 | |
| Amezaliwa | 26 Novemba 1990 Pristina, Yugoslavia ya Kisoshalisti (sasa Kosovo) |
|---|---|
| Nchi |
|
| Elimu | Shule ya Maigizo ya Sylvia Young |
| Kipindi | 2004–sasa |
| Mahusiano | Besim Sahatçiu (babu) |
| Tovuti | ritaora.com |
Rita Sahatçiu Ora (alizaliwa Pristina, Kosovo, 26 Novemba 1990) ni mwimbaji, mwandishi wa nyimbo, haiba wa televisheni, na mwigizaji wa Uingereza. Alipata umaarufu mkubwa mnamo mwaka 2012 baada ya kushirikishwa kwenye wimbo wa DJ Fresh uitwao "Hot Right Now", ambao ulishika nafasi ya kwanza kwenye chati za muziki za Uingereza. Mnamo mwaka 2008, alisaini mkataba wa kazi na lebo ya rapa wa Marekani Jay-Z iitwayo Roc Nation na kutoa albamu yake ya kwanza ya studio, Ora mwaka (2012), ambayo ilianza kwa kushika nafasi ya kwanza kwenye Chati ya Albamu za Uingereza na kutoa nyimbo zilizoshika nafasi ya kwanza nchini humo kama vile "R.I.P." na "How We Do (Party)".
Mnamo mwaka 2014, Ora alishirikishwa kwenye wimbo wa rapa wa Australia, Iggy Azalea uitwao "Black Widow", ambao ulishika nafasi ya tatu kwenye chati ya Marekani ya Billboard Hot 100. Mwaka uliofuata, aliteuliwa kuwa balozi wa heshima wa nchi ya Kosovo. Baada ya kuondoka Roc Nation, Ora alisaini mkataba na Atlantic Records na kutoa albamu yake ya pili ya studio, Phoenix (2018). Albamu hii ilitoa nyimbo maarufu kama "Your Song", "Anywhere", na "Let You Love Me", ambapo wimbo wa mwisho ulimfanya Ora kuwa msanii wa kwanza wa kike wa kujitegemea kutoka Uingereza kuwa na jumla ya nyimbo kumi na tatu zilizowahi kuingia kwenye kumi bora nchini Uingereza. Albamu yake ya tatu ya studio, You & I ya mwaka (2023), ilianza kwa kushika nafasi ya sita nchini Uingereza.
Ora amekuwa jaji kwenye mashindano ya televisheni ya kutafuta vipaji ikiwa ni pamoja na The X Factor UK (2015), The Masked Singer UK (2020–2024), na The Masked Singer US (2024–sasa), pamoja na kuwa kocha kwenye mashindano ya The Voice UK (2015) na The Voice Australia (2021–2023). Pia alicheza uhusika wa Mia Grey katika mfululizo wa filamu za Fifty Shades (2015–2018).
Maisha ya mapema
[hariri | hariri chanzo]Rita Sahatçiu alizaliwa tarehe 26 Novemba 1990 huko Pristina, nchini Yugoslavia (sasa ni Kosovo), akiwa na wazazi wenye asili ya Albania.[1][2] Mama yake,anayeitwa Vera , ni daktari wa magonjwa ya akili na baba yake, Besnik Sahatçiu, ni mmiliki wa baa ambaye alisomea mambo ya uchumi.[3] Mama yake Ora ni muumini wa Kanisa Katoliki na baba yake ni Muislamu.[3] Ora ana dada mkubwa anayeitwa Elena, na kaka mdogo anayeitwa Don. Babu yake mzaa mama, Osman Bajraktari, alikuwa balozi mdogo wa Albania nchini Urusi (wakati huo ikiwa sehemu ya Umoja wa Kisovieti).[4][5] Babu yake mzaa baba, Besim Sahatçiu, alikuwa mwongozaji wa filamu na michezo ya kuigiza.[6][7] Jina la ukoo Sahatçiu linatokana na neno la Kituruki linalomaanisha "mwenye kutengeneza saa"; baadaye wazazi wake waliongeza neno Ora (ambalo kwa Kialbania linamaanisha "muda" au "saa") kwenye jina la ukoo ili liweze kutamkwa kwa urahisi.[8][9]
Familia yake iliondoka Kosovo kwa sababu za kisiasa, kutokana na mateso dhidi ya Waalbania yaliyoanza wakati wa kusambaratika kwa nchi ya Yugoslavia.[10] Walihamia London mnamo mwaka 1991, wakati Ora akiwa bado mtoto mchanga.[3] Alikulia katika eneo la Notting Hill huko Magharibi mwa London nchin Uingereza[11] na kusoma kwenye shule ya sanaa za maonesho iitwayo Sylvia Young Theatre School.[12][13][14]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Jeffries, David. "Rita Ora". AllMusic. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Septemba 2015. Iliwekwa mnamo 29 Mei 2017.
Born in Pristina, Kosovo but raised in London, pop star Rita Ora
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Rita Ora on Apple Music". Apple Music. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Mei 2023. Iliwekwa mnamo 1 Mei 2023.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 3 Taro Greenfeld, Karl. "Rita Ora Interview – July 2015 Cover Story". Marie Claire (July 2015 issue).
And that was enough, apparently, to lure their Muslim father, Besnik (Vera is Catholic). The two fled conflict–torn Kosovo in 1991, when Ora was a year old, and settled in London. Her father, who had studied economics, opened his pub–he's not a devout Muslim–and her mother became a psychiatrist.
- ↑ "Nëna e Rita Orës "pushton" ballinat botërore" (kwa Kialbania). indeksonline.net. 16 Aprili 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 30 Desemba 2015.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Gjergji, Seremb (5 Septemba 2013). "Tri femrat që na shndrisin" (kwa Kialbania). seremb.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 30 Desemba 2015.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Mills, Simon (1 Februari 2013). "Rita Ora: 'You have to make yourself... unforgettable'". London Evening Standard. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Oktoba 2013. Iliwekwa mnamo 20 Julai 2013.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Flet babai, Besnik Sahatçiu: Të pathënat drug jeta e Rita Orës që nga mosha njëvjeçare". Telegrafi (kwa Kialbania). 5 Juni 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Juni 2018. Iliwekwa mnamo 17 Juni 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Keegan, Simon (11 Januari 2015). "Rita Ora's rags to riches story as Voice judge's family fled oppression in Kosovo". Daily Mirror. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Aprili 2018. Iliwekwa mnamo 2 Aprili 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Huntington, Patty (23 Machi 2022). "Rita Ora on farewelling Australia and discovering new directions". Harper's Bazaar Australia. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Machi 2022. Iliwekwa mnamo 24 Machi 2022.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Longmire, Becca (10 Mei 2012). "Rita Ora Reveals Traumatic Refugee Past". entertainmentwise.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Oktoba 2015. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2015.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Rita Ora's My London". London Evening Standard. 31 Agosti 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Februari 2018. Iliwekwa mnamo 4 Novemba 2012.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Sylvia Young Theatre School: Preparing students with raw talent to be the stars of tomorrow". The Stage (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Februari 2021. Iliwekwa mnamo 1 Februari 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Lipkin, Simon (31 Julai 2025). "This teacher shaped Amy Winehouse and Rita Ora — she changed my life". www.thetimes.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 17 Septemba 2025.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Stage school founder Sylvia Young, who helped discover Amy Winehouse, dies | ITV News". ITV News (kwa Kiingereza (Uingereza)). 30 Julai 2025. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Julai 2025. Iliwekwa mnamo 17 Septemba 2025.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu wakimbizi au masuala ya ukimbizi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Rita Ora kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
| Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Ulaya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Rita Ora kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |