Río Muni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Rio Muni)
Río Muni

Río Muni (inaitwa pia Mbini kwa lugha ya Kifang, au Región Continental kwa Kihispania ) ni moja ya kanda mbili za Guinea ya Ikweta. Inajumuisha eneo la bara la nchi hiyo likiwa na kilomita za mraba 26,017.

Jina hilo limetokana na Mto Muni, ambako Wazungu wa kwanza waliofika hapa walijenga makazi.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Pwani la Río Muni ilikuwa chini ya Ureno iliyoikabidhi kwa

Hispania mnamo 1778 katika Mkataba wa El Pardo . Wahispania walikuwa na matumaini ya kununua watumwa kwa koloni za huko Marekani. Lakini walowezi wengi walikufa kwa homa ya manjano, na eneo hilo lilibaki bila walowezi.

Baadaye Wahispania walirudi na kuanzisha mashamba ya kakao pamoja na kuvuna mbao ambazo zilikuwa tasnia kuu. Río Muni, pamoja na Bioko, ikawa mkoa wa Guinea ya Kihispania mnamo 1959.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka wa 2015 Rio Muni ilikuwa na watu 885,015 ambao walikuwa 72% ya wakazi wote wa Guinea ya Ikweta. Lugha kuu zinazozungumzwa katika Río Muni ni Kifang cha Ntumu, ambacho kinazungumzwa kwenye kaskazini, na Kifang cha Okak, ambacho kinazungumzwa kusini. Kihispania kinatumiwa pia na wengi kama lugha ya pili na lugha ya mawasiliano.

Mikoa[hariri | hariri chanzo]

Río Muni inajumuisha majimbo matano:

Miji[hariri | hariri chanzo]

Jiji kubwa zaidi ni Bata, ambalo pia hutumika kama mji mkuu wa kiutawala wa mkoa. Miji mingine mikuu ni pamoja na Evinayong, Ebebiyín, Acalayong, Acurenam, Mongomo na Mbini .

Marejeo[hariri | hariri chanzo]