Rigathi Gachagua

Geoffrey Rigathi Gachagua (alizaliwa 28 Februari 1965) ni mwanasiasa wa nchini Kenya ambaye tangu mnamo 2022 alihudumu kama Naibu Rais wa nchi hiyo chini ya Rais William Ruto kabla ya kutolewa madarakani mnamo Oktoba 2024[1].
Pia alikuwa Mbunge wa jimbo la Mathira kuanzia 2017 hadi 2022. Gachagua ni miongoni mwa wanasiasa wenye ushawishi mkubwa kutoka eneo la Mlima Kenya.
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Gachagua alizaliwa katika familia ya Nahashon Gachagua Reriani na Martha Kirigo katika Kaunti ya Nyeri. Familia yao ilikuwa miongoni mwa waliounga mkono Mau Mau wakati wa harakati za uhuru wa Kenya.[2]
Alisoma katika shule ya msingi ya Kabiruini, kisha akajiunga na Shule ya Upili ya Kianyaga. Baadae alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi akiwa na Shahada ya sayansi ya siasa na utawala wa umma.
Baada ya chuo kikuu (2001 -2006), alihudumu kama katibu binafsi wa George Saitoti, Waziri wa mambo ya ndani.[3] Baadae alijihusisha na biashara binafsi hasa za huduma na usambazaji wa vifaa serikalini, jambo ambalo lilizua maswali kuhusu uhalali wa mali zake.
Maisha ya siasa
[hariri | hariri chanzo]Gachagua alichaguliwa kuwa Mbunge wa Mathira mwaka 2017 kwa tiketi ya Chama cha Jubilee. Alijitokeza kuwa mkosoaji wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta na kuwa mfuasi wa karibu wa William Ruto.
Mnamo mwaka 2022, aliteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Ruto kupitia muungano wa Kenya Kwanza. Baada ya ushindi katika uchaguzi wa urais, alikula kiapo kuwa Makamu wa Rais mnamo 13 Septemba 2022.
Mijadala na utata
[hariri | hariri chanzo]Gachagua amekuwa akizua mijadala kutokana na kauli zake kuhusu ugavi wa rasilimali na siasa za kikanda. Pia alikumbwa na kesi ya madai ya utakatishaji fedha ambapo mahakama iliagiza fedha zaidi ya KSh 200 milioni zikabidhiwe kwa serikali, ingawa alikanusha na kusema ni njama za kisiasa.
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Gachagua ameoa mkewe Dorcas Rigathi, ambaye ni mchungaji. Wana watoto wawili. Ameshikilia msimamo wa kidini na maadili ya kifamilia katika maisha yake ya kisiasa.[2]
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Vivianne Wandera. "Kenya Deputy President Rigathi Gachagua impeached: Why it matters". Al Jazeera (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-07-19.
- 1 2 "Who is Rigathi Gachagua?". Daily Nation. 19 Julai 2022. Iliwekwa mnamo 19 Julai 2025.
- ↑ "Rigathi Gachagua: The man who defied Uhuru to back Ruto". The Standard. 15 Julai 2022. Iliwekwa mnamo 19 Julai 2025.
| Makala hii kuhusu mwanasiasa huyo wa Kenya bado ni mbegu. Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |