Nenda kwa yaliyomo

Richard Mofe-Damijo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Richard Mofe-Damijo

Chifu Richard Evans Mofe-Damijo (alizaliwa 1961), anajulikana kama RMD,[1][2]  ni mwigizaji, mwandishi, mtayarishaji, wakili, na mwandishi wa habari wa zamani kutoka Nigeria.[3] Alihudumu kama Kamishna wa Utamaduni na Utalii katika Jimbo la Delta kuanzia mwaka 2009 hadi  mwaka 2015.[4][5][6] Mofe-Damijo alishinda Tuzo za Akademia ya Filamu Afrika kama Muigizaji Bora katika Nafasi ya Uongozi mwaka 2005.[7][8] Alipokea Tuzo ya Mafanikio ya Maisha katika Tuzo za 12 za Akademia ya Filamu Afrika mwaka 2016.[9][10] Mnamo mwaka 2024, alitunukiwa Tuzo za Ustahimilifu wa Sekta, pamoja na Iya Rainbow katika Tuzo za Chaguo la Watazamaji wa Africa Magic.[11]

Maisha ya Awali

[hariri | hariri chanzo]

Mofe-Damijo alizaliwa katika mji wa Aladja, Ufalme wa Udu, ambalo kwa sasa ni Jimbo la Delta. Alihudhuria Chuo cha Midwest, Warri na Shule ya Sarufi ya Anglikana, ambapo alikuwa mwanachama wa klabu ya maigizo. Alisoma sanaa ya maigizo katika Chuo Kikuu cha Benin,[3] na baadaye akasoma sheria katika Chuo Kikuu cha Lagos, na kuhitimu mwaka 2004.[7]

Baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu akiwa na shahada ya sanaa ya uigizaji, Mofe-Damijo alionekana katika tamthila ya televisheni Ripples kama mkaguzi wa polisi lakini alipata umaarufu zaidi kama mhalifu Segun Kadiri katika filamu pinzani ya Checkmate. Kabla ya hapo, alikuwa mwandishi katika gazeti la kila siku la The Concord, na majarida ya Metro and Quality.[12]Out of Bounds ilikuwa filamu ya kwanza ambayo ilimpatia sifa kama mwandishi na mtayarishaji.[3] Mnamo mwaka 2005, katika toleo la kwanza la Tuzo za Akademia ya Filamu Afrika, Mofe-Damijo alishinda tuzo ya Muigizaji Bora katika nafasi ya uongozi.[7] Mnamo mwaka 2017, aliandaa Tuzo za GLO-CAF ya mwaka 2016 pamoja na mwandishi wa habari wa Nigeria anyeitwa Mimi Fawaz.[13] Mnamo mwaka 2021, alipokea Tuxo ya Black Star Honor katika hafla ya Rhymes on Da Runway huko Accra, Ghana.[14]

Kazi ya Kisiasa

[hariri | hariri chanzo]

Mofe-Damijo aliteuliwa kuwa Mshauri Maalum wa Utamaduni na Utalii[15] kwa Gavana Emmanuel Uduaghan wa Jimbo la Delta, mnamo mwaka 2008. Baadaye alihudumu kama Kamishna wa Utamaduni na Utalii katika Jimbo la Delta kuanzia maka 2009 hadi mwaka 2015.[8][16]

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Mofe-Damijo alimuoa Mary Ellen 'MEE' Ezekiel,ambaye ni mwandishi wa habari, mchapishaji na mtangazaji wa kipindi cha mazungumzo.[17] Baada ya kifo chake mwaka 1996, Mofe-Damijo alimuoa Jumobi Adegbesan, ambaye ni mtangazaji maarufu wa televisheni. Baadaye aliacha utangazaji na kujiunga na sekta ya makampuni. RMD ana watoto watano.[18]

  1. akintayo eribake (2014-07-25). "RMD set to get Chieftaincy title at Igbo film festival". Vanguard News (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2026-04-11.
  2. Vama Saini (2025-10-29). "RMD in Calgary: A four-day cultural event". The Gauntlet (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-04-11.
  3. 1 2 3 https://web.archive.org/web/20201013033028/https://www.newswatchngr.com/editorial/allaccess/special/10112232035.htm/
  4. Alausa-Issa Zainab (2024-05-14). "10th AMVCA: 10 facts about Industry Merit Award winner, Richard Mofe-Damijo". Tribune Online (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2026-04-11.
  5. "Richard Mofe-Damijo (RMD): A comprehensive biography". Pulse Nigeria (kwa Kiingereza). 2025-02-27. Iliwekwa mnamo 2026-04-11.
  6. Ameh Comrade Godwin (2012-11-30). "Former Nollywood actor, Richard Mofe-Damijo in N50m embezzlement scandal". Daily Post Nigeria (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-04-11.
  7. 1 2 3 https://thenationonlineng.net/web2/articles/26859/1/New-world-of-A-list-stars-blacklisted-in-2005/Page1.html#google_vignette
  8. 1 2 "Wayback Machine". media.deltastateonline.com. Iliwekwa mnamo 2026-04-11.[dead link]
  9. "For RMD, It's Good News from Kigali – THISDAYLIVE" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-04-11.
  10. "RMD receives Lifetime Achievement award from Pete Edochie (AMAA 2016)", Nollywood Community (kwa American English), 2016-06-14, iliwekwa mnamo 2026-04-11
  11. Our Reporters (2024-05-12). "AMVCA 2024: Iya Rainbow, RMD bag Lifetime awards as Bankole, Ojo win best actors". Punch Newspapers (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-04-11.
  12. punchng (2018-09-15). "After Concord Newspaper died, it felt like I lost a baby –Mike Awoyinfa". Punch Newspapers (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-04-11.
  13. "News". News (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2026-04-11.
  14. "Richard Mofe-Damijo honoured in Ghana" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-04-11.
  15. "SPECIAL ADVISER OR NOT, I'M STILL AN ACTOR — RMD". Nigerian Voice. Iliwekwa mnamo 2026-04-11.
  16. "Nigeria: MC Olokpa Bombs RMD", allAfrica.com (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2026-04-11
  17. Anthony (2017-03-25). "Remembering May Ezekiel, 21 years after". The Guardian Nigeria News - Nigeria and World News (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2026-04-11.
  18. "RMD: Two Decades of Screen Romance". nigeriamovies.net. Iliwekwa mnamo 2026-04-11.