Nenda kwa yaliyomo

Richard Dawkins

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Richard Dawkins (alizaliwa Nairobi, Kenya, 26 Machi 1941) ni mwanabiolojia wa mageuzi na mwandishi kutoka Uingereza. Amekuwa profesa katika Chuo Kikuu cha Oxford na mshirika wa New College. Dawkins anajulikana kwa kitabu chake The Selfish Gene kilichotoka mwaka 1976, ambacho kilieleza kuwa Jenetikia ndizo msingi wa mageuzi na ndipo alipoanzisha neno “meme” kwa kueleza jinsi mawazo na utamaduni huenea kama Jenetikia. Ameandika vitabu vingine vingi vya sayansi na dini, na amekuwa akihamasisha watu kuelewa sayansi kwa urahisi. Dawkins pia amepata tuzo nyingi kutokana na mchango wake katika uandishi na mawasiliano ya kisayansi.[1][2]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kuhamia Uingereza alisoma zoolojia na kupata PhD mwaka 1966 chini ya Nikolaas Tinbergen. Dawkins alipata umaarufu kwa kitabu The Selfish Gene (1976), kilichotambulisha neno “meme,” na The Blind Watchmaker (1986), ambacho kilipinga hoja ya muumbaji. Mwaka 2006 aliandika The God Delusion, akisema Mungu hayupo na dini ni udanganyifu. Dawkins ni mkosoaji mkubwa wa imani ya uumbaji na dini. Ameanzisha taasisi ya kusaidia sayansi na ameandika vitabu vingi vilivyopata umaarufu duniani.[3][4][5][6][7]

  1. "Richard Dawkins". London: Royal Society. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 23 Aprili 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Tortoise (2 Desemba 2019). OMG – A ThinkIn with Richard Dawkins. YouTube. Tokeo mnamo 2:08. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Desemba 2021. Iliwekwa mnamo 31 Januari 2020.{{cite AV media}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Fahy, Declan (2015). The New Celebrity Scientists: Out of the Lab and into the Limelight. Rowman & Littlefield Publishers.
  4. "British scientists don't like Richard Dawkins, finds study that didn't even ask questions about Richard Dawkins". Independent.co.uk. 18 Januari 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Juni 2020. Iliwekwa mnamo 26 Juni 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Elmhirst, Sophie (9 Juni 2015). "Is Richard Dawkins destroying his reputation?". The Guardian.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)(Op-ed)
  6. "Richard Dawkins on Charles Darwin". BBC News. 14 Februari 2009.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Holt, T. "Richard Dawkins". Philosophy of Religion. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2025-01-19. Iliwekwa mnamo 2025-03-05.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Richard Dawkins kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.