Richard Akuson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Richard Akuson (alizaliwa Julai 26, mwaka 1993) ni wakili wa Nigeria, mwanaharakati wa haki za wasagaji na mashoga, mwandishi, mhariri, na mwanzilishi wa jarida la A Nasty Boy [1], chapisho la kwanza la LGBTQ+ nchini Nigeria. Kufuatia kuzinduliwa kwa jarida la A Nasty Boy mwaka wa 2017, alitajwa kuwa mmoja wa Wanaijeria 40 Wenye Nguvu Zaidi chini ya umri wa miaka 40 na YNaija. [2]

Maisha yake na Elimu[hariri | hariri chanzo]

Richard Akuson alizaliwa Akwanga, katika Jimbo la Nasarawa, nchini Nigeria. Ni kijana wa pili kati ya watatu, alilelewa katika familia ya tabaka la juu; baba yake, mwanasiasa, na mama yake, mhadhiri wa chuo kikuu. Alisoma Shepherd's International College, shule binafsi ya bweni ya Kikristo, kabla ya kuelekea Chuo Kikuu cha Jimbo la Nasarawa, Keffi, kwa shahada yake ya kwanza ya taaluma ya sheria. Aliitwa kwenye Baa ya Nigeria kama Mwanasheria na Wakili wa Mahakama Kuu ya Nigeria mwaka wa 2017, baada ya kuhitimu kutoka Shule ya Sheria ya  jijini Lagos nchini Nigeria.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Matadeen, Priya (2022-05-27), "Dazed Media", Insights on Fashion Journalism (Routledge): 88–93, ISBN 978-1-003-03568-8, iliwekwa mnamo 2022-09-24 
  2. "Pricing Beauty", Pricing Beauty (University of California Press), 2019-12-31: iii–vi, iliwekwa mnamo 2022-09-24 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Richard Akuson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.