Reuben Kosgei

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rekodi za medali
Anawakilisha nchi Bendera ya Kenya Kenya
Men’s Wanariadha
Olympic Games
Dhahabu 2000 Sydney 3000 m steeplechase
World Championships
Dhahabu 2001 Edmonton 3000 m steeplechase
Commonwealth Games
Medali ya Shaba 2006 Melbourne 3000 m steeplechase

Reuben Seroney Kosgei (Alizaliwa 2 Agosti 1979) ni mwanariadha wa Kenya wa masafa ya Kati na Masafa Marefu.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa katika wilaya ya Kapsabet, Kenya mnamo 1979

Kazi yake ya Riadha[hariri | hariri chanzo]

Anajulukana kwa umaarufu wake katika shindano la mita 3000 kuruka viunzi na kidimbwi cha maji ambapo aliwahi kuwa mshindi wa nishani ya Dhahabu mwenye umri mdogo zaidi katika Ollimpiki wakati alishinda shindano hili jijini Sydney mnamo 2000 akiwa na umri wa miaka 19 peke yake. Hata hivy, muda wake wa ushindi huo, 8:21:43 ulikuwa muda wa kasi ya chini zaidi katika hisoria ya shindano hilo tangu Mashindano ya Olimpiki ya 1972

Alikuwa mmoja wa wale waliopokea shutma kwa kukosa kushiriki katika katika Mashindano ya Jumuia ya Madola ya 2002 na badala yake wakaamua kufuata madola yaliyokuwa yameahidiwa katika Ligi ya IAAF. Wengine ni Richard Limo na Bernard Lagat.

Katika Mashindano ya Jumuia ya Madola ya 2006, hata hivyo, alishinda nishani ya Shaba katika shindano lilo hilo la mita 3000 kuruka viunzi.

Alishiriki katika shindano la Marathon kwa mara ya kwanza mnamo 2009 katika Mashindano ya Vienna Marathon lakini hakumaliza mbio hizo. Alimaliza wa pili katika Mashindano ya Florence Marathon ya 2009[1]

Mafanikio Muhimu[hariri | hariri chanzo]

(zifuatazo zote ni katika shindano la 3000m Kuruka Viunzi)

Virejeleo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu Mwanariadha wa Kenya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Reuben Kosgei kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.