Nenda kwa yaliyomo

Kabumbu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Remizidae)
Kabumbu
Kabumbu uso-njano
Kabumbu uso-njano
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Remizidae (Ndege walio na mnasaba na kabumbu)
Olphe-Galliard, 1891
Ngazi za chini

Jenasi 3, spishi 12:

Kabumbu ni ndege wadogo wa familia Remizidae. Wanafanana na domofupi lakini domo lao ni jembamba zaidi lenye ncha kali zaidi. Mabawa yao ni mafupi na yameviringa, na mkia una mkato wa V mwishoni. Wana rangi ya kijivu pamoja na njano na nyeupe na pengine nyeusi au nyekundu. Wanatokea Afrika, Asia, Ulaya na Amerika ya Kaskazini katika maeneo yenye miti. Hula wadudu. Tago lao lina umbo wa pea, hujengwa kwa nywele za wanyama, nyuzinyuzi za mimea na utando wa buibui, na huning'inizwa kutoka kitawi, mara nyingi juu ya maji, na mwingilio uko kando yake. Kabumbu wa Afrika hutengeneza mwingilio mdanganyifu juu ya mwingilio wa kweli unaoelekea katika chumba kidanganyifu. Mwingilio wa kweli umefunikwa. Tago la Auriparus hujengwa kwa vitawi vyenye miiba.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine

[hariri | hariri chanzo]