Mikoa ya Mali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Regions of Mali)
Ramani ya Mali (ugawaji kabla ya mwaka 2016)

Mikoa ya Mali ni magatuzi ya nchi ya Mali kwenye ngazi ya juu. Tangu mwaka 2016 Mali imegawanywa katika mikoa kumi na eneo la pekee la mji mkuu.

Mnamo mwaka 2012 sheria ilitangaza kugawiwa upya kwa nchi katika mikoa 19 kutoka ile 8 ya awali[1]. Hadi mwaka 2021 kuna mikoa miwili mipya pekee iliyoanzishwa, ambayo ni Taoudenit (iliyomegwa kutoka Mkoa wa Timbuktu) na Menaka (zamani kwenye Mkoa wa Gao).[2] [3]

Kila mkoa unaitwa jina la mji mkuu wake. Mikoa imegawanywa katika wilaya (cercles) 56. Wilaya zote zimegawanywa katika manispaa (communes) 703. [4]

Jiografia

Mikoa 5 ni hasa jangwa, na mikoa hiyo ina nusu ya eneo lote la nchi.

Mkoa mkubwa zaidi ni Taoudenit, mdogo zaidi ni Segou.

Demografia

Mkoa wenye watu wengi zaidi ni Sikasso wenye watu milioni 2.6, na ule wenye watu wachache zaidi una watu 68,000 pekee.

Mikoa

Mikoa imepewa namba kwa kutumia namba za Kiroma.[5] Mji mkuu wa Bamako unasimamiwa kama eneo la pekee.

Mikoa kumi na eneo la Bamako vimeorodheshwa hapa chini. Idadi ya wakazi ni kutokana na sensa za 1998 na 2009. [6]

A map of former regions of Mali
Mikoa ya Mali (mnamo 2016)
Jina la mkoa Nambari ya mkoa Eneo (km2) Idadi ya watu
Sensa ya 1998
Idadi ya watu
Sensa ya 2009
Kayes I 119,743 1,374,316 1,993,615
Koulikoro II 95,848 1,570,507 2,422,108
Bamako (bila namba) 252 1,016,296 1,810,366
Sikasso III 70,280 1,782,157 2,643,179
Segou IV 64,821 1,675,357 2,338,349
Mopti V 79,017 1,484,601 2,036,209
Timbuktu[7] VI 496,611 442,619 674,793
Gao VII 89,532 341,542 542,304
Kidal VIII 151,430 38,774 67,739
Taoudénit IX - - -
Ménaka X 81,040 - -

Marejeo

  1. LOI No 2012-017 DU 02 MARS 2012 PORTANT CREATION DE CIRCONSCRIPTIONS ADMINISTRATIVES EN REPUBLIQUE DU MALI. Journal officiel de la République du Mali (2 March 2012). Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-11-23. Iliwekwa mnamo 21 February 2017.
  2. Régionalisation: Deux Nouvelles régions créées au Mali. Malijet (21 January 2016). Jalada kutoka ya awali juu ya 2017-02-22. Iliwekwa mnamo 21 February 2017.
  3. Report of the Secretary-General on the situation in Mali. MINUSMA (28 March 2016). Iliwekwa mnamo 21 February 2017.
  4. Loi N°99-035/ Du 10 Aout 1999 Portant Creation des Collectivites Territoriales de Cercles et de Regions (in French), Ministère de l'Administration Territoriales et des Collectivités Locales, République du Mali, 1999, archived from the original on 2012-03-09 .
  5. Évaluation de la coopération décentralisée franco-malienne La coopération décentralisée franco-malienne, état des lieux Archived 14 Februari 2012 at the Wayback Machine., Ministère des Affaires étrangères et européennes (French Ministry of Foreign Affairs).
  6. Resultats Provisoires RGPH 2009 (in French), République de Mali: Institut National de la Statistique, archived from the original on 2020-01-11, retrieved 2022-01-09 .
  7. Namba za Timbuktu bado pamoja na eneo na wakazi wa mkoa mpya wa Taoudenit uliotengwa hapa mwaka 2016