Nenda kwa yaliyomo

Regina Daniels

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Regina Daniels (alizaliwa Oktoba 10, 2000) [1] ni mwigizaji na mtayarishaji wa filamu kutoka nchini Nigeria. [2]

Akiwa mwigizaji mdogo wa kike, aliigiza kama Onyeure katika filamu ya kuigiza ya Dumebi in School (2014), Kenya Obi katika Merry Men 2 (2019), na aliitwa Yewande katika filamu ya kupigana ya Hakeem: Seeking Justice (2025).

Regina Daniels alizaliwa jijini Lagos, Lagos State, Nigeria mnamo tarehe 10 October 2000. Mama yake anaitwa Rita Daniels, ni mtayarishaji wa filamu na mfanyabiashara na baba yake anaitwa Jude Ojegwu. Alikulia maeneo ya Asaba, Delta State pamoja na ndugu zake watano, wa kiume watatu na wa kike wawili.

Regina alipata shahada yake ya kwanza ya mawasiliano ya umma katika chuo kikuu cha Igbinedion mwaka 2018. Mwaka 2024 alipata shahada ya saikolojia kutoka chuo kikuu cha Azteca nchini Mexico.

  1. "Actress Regina Daniels Celebrates 17th Birthday With Lovely Photos". National Mirror Online (kwa American English). 2017-10-10. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Februari 13, 2019. Iliwekwa mnamo 2019-05-07.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Regina Daniels: As a 17-year-old Actress, I Earned N500,000 for a Role". Julai 23, 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Aprili 30, 2019. Iliwekwa mnamo Aprili 28, 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Regina Daniels kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.