Reem Bassiouney
Reem Bassiouney (Kiarabu cha Kimsri: ريم بسيونى Rīm Basyūni [ɾiːm bæsˈjuːni]; alizaliwa 6 Machi 1973) ni mwandishi wa Misri, profesa wa isimu jamii, na Mwenyekiti wa Idara ya Isimu Tumikizi katika Chuo Kikuu cha Marekani kilichoko Cairo[1].
Zaidi ya hayo, Bassiouney ni mhariri wa Routledge Series of Language and Identity[2]. Pia ni mhariri na mwanzilishi wa jarida Arabic Sociolinguistics Edinburgh
Ameandika riwaya kadhaa na hadithi fupi nyingi, na alishinda Tuzo ya Fasihi ya Sawiris Foundation ya Waandishi Vijana mwaka 2009 kwa riwaya yake Dr. Hanaa. Ingawa sehemu kubwa ya kazi zake za kifasihi bado haijatafsiriwa kwa Kiingereza, riwaya yake The Pistachio Seller ilichapishwa na Syracuse University Press mwaka 2009.
Elimu na Kazi
[hariri | hariri chanzo]Reem Bassiouney alizaliwa mjini Alexandria mwaka 1973. Alisoma katika El Nasr Girls' College, na baadaye akasomea fasihi ya Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Alexandria. Baada ya kuhitimu, aliteuliwa kufanya kazi katika chuo hicho, lakini aliamua kuendeleza masomo yake nje ya nchi. Alikubaliwa kujiunga na programu ya shahada ya uzamili katika isimu katika Chuo Kikuu cha Oxfor.ambapo alijiunga na Somerville College. Alipata shahada yake ya uzamivu (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha Oxford, na alifanya kazi kwa muda mfupi nchini Uingereza.
Maktaba ya Kazi Zake
[hariri | hariri chanzo]Fasihi ya Kubuni
- Harufu ya Bahari (The Smell of the Sea), 2005 – رائحة البحر
- Muuzaji wa Pistachio (The Pistachio Seller), 2007 – بائع الفستق
- Tafsiri ya Kiingereza, 2009
- Mshindi wa Tuzo ya Tafsiri ya Fasihi ya Kiarabu ya Kituo cha Mfalme Fahd cha Masomo ya Mashariki ya Kati na Kiislamu, 2009
- Dkt. Hanaa (Dr. Hanaa), 2008 – دكتورة هناء
- Mshindi wa Tuzo ya Fasihi ya Sawiris Foundation kwa Waandishi Vijana, 2009
- Tafsiri ya Kiingereza, 2011
- Pia imetafsiriwa kwa Kihispania na Kigiriki
- Mapenzi kwa Mtindo wa Kiarabu (Love, Arab Style), 2009 – الحب على الطريقة العربية
- Mchoro wa Maisha (Mortal Designs), 2010 – أشياء رائعة
- Mwongoza Watalii (The Tour Guide), 2010 – مرشد سياحي
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Reem Bassiouney kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |